“Prezzo sio mwanamuziki. Namuona kama model kwakuwa ameshinda category ya Best Dressed katika tuzo za Chaguo La Teeniez mara moja, basi!
Alisema Jaguar katika mahojiano na The Citizen.
“Prezzo hawezi kuongea kuhusu hela kwasababu ntamuumbua katika kitengo hicho hasa pale tutakapoamua kutangaza mali zetu".
Jaguar ambaye jina lake halisi ni Charles Njagua amesema utajiri wake hautegemei muziki peke yake bali yeye ni mfanyabiashara aliyefanikiwa.
Amesema anamiliki gereji ya kisasa inayoitwa Jagz Auto iliyopo mjini Nairobi, kampuni ya taxi iitwayo Jagz cabs na kampuni ya ulinzi iitwayo Jagz Security.
Alipoulizwa kuhusu mahala alipopata fedha hizo Jaguar amesema amehangaika mno mpaka kufika hapo alipo.
“Niliwahi kuwa konda wa Matatu (DalaDala) ili kujilipia ada ya shule. Nilivaa kiatu cha kwanza maishani mwangu nikiwa na miaka 14”.
Amesema Mama yake alifariki wakati akiwa mdogo na Baba yake hakuwajali. "Ilibidi tujilee wenyewe. Nilifanya kila kazi ili kuishi na kupata elimu iliyonifikisha hapa nilipo leo hii”
Amesema alipoanza kufanya muziki, ilikuwa kazi ngumu na alipopata nafasi ya kwenda Marekani, aliweza kutunza fedha na kununu gari yake ya kwanza. “Niliitumia gari hiyo kama taxi na hivyo ndivyo biashara yangu ilianza kukua”.
Mwezi uliopita Jaguar alipata tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kwa wimbo wake Kigeugeu katika tuzo za Kili.
Courtesy of The Citizen
No comments:
Post a Comment