Monday, May 28, 2012

Mlipuko wa bomu Nairobi: Nonini alitabiri, ashuhudia




Wakati jiji la Nairobi leo likiwa kwenye hofu kubwa kutokana na kutokea mlipuko wa bomu mitaa ya Moi Avenue, mwanamuziki wa genge Nonini amesema alikuwa kwenye jengo jirani wakati tukio hilo likitokea ambapo alisikia kishindo.

“Yaani was just hapo imenti house the building shook! Kushtuka after explosion...waaaa.” ametweet.

Katika kile anahisi kama utabiri juu ya tukio hilo jumatatu hii Nonini amesema, “funny enough was with family over the weekend watching jichopevu & told my mum don't be surprised if something major happens on Monday.”


Moi Avenue near the Mount Kenya University

Moi Avenue
Kutokana na kulikupa kwa bomu hilo watu 20 wamelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta baada ya kujeruhiwa.

Majengo kadhaa yaliyopo Moi Avenue, mitaa iliyopo busy jijini Nairobi, yameharibiwa vibaya.


Kumekuwepo na matukio ya kulipuka kwa mabomu jijini Nairobi na Mombasa ambayo yanadaiwa kufanywa na wanamgambo wa kiislam wa kundi Al-shabab tangu majeshi ya Kenya yawashambulie nchini Somalia October mwaka jana.

No comments:

Post a Comment