Wednesday, May 23, 2012

Nas: Michelle Obama ni mwanamke mrembo zaidi duniani



Rapper Nas amesema First Lady wa Marekani Michelle Obama ni mwanamke mrembo zaidi duniani.

Katika mahojiano Nas amesema  "Michelle Obama ni mwanamke mrembo zaidi kwenye sayari ya Dunia. Anajali watu. Mafirst lady wote wana kazi za kufanya lakini yeye ni rahisi kuona alivyodhamiria”


Michelle anamvutia pia mwanamuziki na mshindi wa tuzo ya Grammy,  Beyonce Knowles-Carter ambaye hivi karibuni alimwandikia barua ya wazi.

"Michelle, ni mfano halisi wa mwanamke shupavu mmarekani mwenye asili ya Afrika. Ni mama mwenye kujali, mke mwenye mapenzi ya dhati wakati huo huo ni  FIRST LADY!!!! Pamoja na pressure, na stress za kumulikwa na darubini- ni mnyenyekevu, mwenye mapenzi na mkweli.

Huijenga na kuilea familia yake wakati huo pia akiwaangalia mamilioni wengine kwa namna nyingi. Michelle, asante sana kwa kila jambo unalolifanya kwetu – Najivunia kuwa na mwanangu anayekua katika ulimwengu ambao ana watu wa kuwaangalia. Love, Beyonce." (Beyonce)

No comments:

Post a Comment