Tuesday, May 22, 2012

Think Like A Man yapigwa marufuku Ufaransa


Filamu ya Think Like A Man imepigwa marufuku kuoneshwa kwenye majumba ya sinema nchini Ufaransa kwakuwa maofisa wanaamini kuwa haina mchanganyiko wa tamaduni mbalimbali na kwamba inahusisha mambo ya watu weusi zaidi.

Filamu hiyo iliyotokana na kitabu cha Steve Harvey kiitwacho Act Like A Lady, Think Like A Man, na kuchezwa na wasanii kama Kevin Hart, Gabrielle Union, Taraji P. Henson na Michael Ealy ilizinduliwa mwezi uliopita.

Pamoja na kuwa na waigizaji wengi wamarekani wenye asili ya Afrika, kwenye filamu hiyo kuna waigizaji wachache wazungu. 

Hata hivyo maafisa wa filamu nchini Ufaransa hawaamini kama kuna mchanganyiko wa kutosha kwenye filamu hiyo na hivyo kuisitisha tarehe ya kuzinduliwa rasmi kwa filamu hiyo nchini humo.

"Waigizaji weusi na movie za watayarishaji kama Tyler Perry huwa hazioneshwi kwenye majumba ya sinema nchini Ufaransa bali huzinduliwa kwenye DVD peke yake licha ya filamu zake kuongoza kwa mauzo kwenye majumba hayo nchini Marekani kwa filamu zake zikiwemo ‘Why did I get Married’ na ‘For Colored Girls’," umeandika mtandao wa GlobalVoicesOnline.

"Jamii ya kifaransa ni ya kinafiki inapokataa kuonesha filamu za watayarishaji weusi ambao hupata mamilioni kwa kuonesha ujumbe muhimu kwa waaafrika waaishio ugenini kupitia filamu zao” uliandika mtandao huo.

No comments:

Post a Comment