Tuesday, May 29, 2012

Habida: Badala ya kukimbia bomu watu wanaenda kushuhudia



Mwafrika ni mwafrika tu haachi asili yake. Mara ngapi umeshuhudia pametokea jambo la hatari na watu hawatakiwi kusogea lakini wengine kwa kutokujua ama ushamba husogea karibu ili kushuhudia kinachoeendelea?

Ndicho kilichotokea jana jijini Nairobi baada ya bomu kulipa mitaa ya Moi Avenue, jambo ambalo halijamuingia akilini mwanadada Habida.

“Ok Kenyans really, why?? ok a bomb goes off and instead of running to a safer place you flock to the area to see what happened? REALLY,” alitweet.

Anashangaa kuona watu wengine wana ujasiri wa namna gani! kwamba badala ya kukimbia kuokoa maisha yao, bila woga husogea eneo la tukio ili kupata cha kusimulia nyumbani.





Hakufurahishwa pia na waziri mkuu Raila Odinga ambaye alienda kwenye eneo la tukio kujionea pia. Habida ameandika, “okay and then our Prime Minister goes to bomb sites, really my people we need to need to focus on priorities. We have police right?”

Hapa kidogo wengi watambishia mrembo huyu kwakuwa vipaumbele anavyovizungumzia ndio hivyo serikali kuwajibika haraka kwa kumpeleka waziri mkuu kujionea hali halisi kufuatia tukio la kigaidi lililoteta hofu kwa wenzetu wa Kenya, au sio jamani?

No comments:

Post a Comment