Thursday, May 31, 2012

Ukweli: Eddie Murphy na Rocsi Diaz wanadate

Eddie Murphy
Eddie Murphy na Rocsi Diaz wamedaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa mwezi mmoja sasa na mpaka hivi karibu walienda holiday kula bata.

Muigizaji huyo wa Tower Heist na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha 106 & Park cha BET, walionekana pamoja wiki iliyopita wakiwa wameshikana mikono baada ya kutoka kunywa kahawa pamoja kiasi cha kuongeza mafuta fununu za uhusiano wao.

Rocsi alikanusha haraka hata hivyo kwa kudai wao ni marafiki tu.



Rocsi Diaz
Hata hivyo vyanzo vimeuambia mtandao wa Eurweb.com kuwa ni kweli wana uhusiano uliodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa na Eddie alimpeleka mrembo huyo kwenye visiwa vya Bahamas kwa ndege ya kukodi (private jet).

No comments:

Post a Comment