Tuesday, May 22, 2012

Beyonce na Jay-Z wagombana, kisa Kim Kardashian


\

Jay-Z na Beyonce wamedaiwa kuwa katika ugomvi mzito kutokana na kutofautiana katika uamuzi wa kumkubalia Kim Kardashian karibu na familia yao.

Ugomvi huo umetokea katika sherehe ya siku za kuzaliwa ya rafiki wa siku nyingi wa Jay-Z aitwaye Ty Ty ambapo Jay na marafiki zake wengine kwa muda mrefu walikuwa wamepanga kumfanyia sherehe mjini London, Uingereza.

Kila kitu kilikuwa safi hadi pale KIM KARDASHIAN alipohusika. Kim alimtaka mpenzi wake Kanye ampeleke kwenye party hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu duniani ambapo Kanye alikubali kufanya hivyo. Hilo likawa tatizo kwa Beyonce.

"Beyonce hakutaka kwenda baada ya kugundua kuwa Kim [Kardashian] naye angehudhuria. Hivyo akamuomba mume wake [Jay Z]kutomruhusu kuja[Kim]. Lakini [Jay] alishindwa kufanya hivyo kwakuwa Kim alikuwa mgeni wa Kanye.” Mtu mmoja ameuambia mtandao wa mediatakeout.com.


Kutokana na hali hiyo Beyonce akagoma kuhudhuria sherehe hiyo.Jay alichukia na kuumia sana kwakuwa Beyonce alikataa kuhudhuria sherehe ya rafiki yake mkubwa duniani Ty Ty ambaye pia ni baba (kidini) wa mtoto wake Blue kisa tu Kim alihudhuria pia.

Tangu Kim Kardashian awe mpenzi wa Kanye, mengi yamekuwa yakizungumzwa iwapo kama Beyonce anaweza kuwa rafiki wa Kim na tayari uwezekano huo umeanza kuingiwa na dosari.

No comments:

Post a Comment