Philips (mzungu), Jessica na Joshua |
Joshua Ledet kipenzi cha wengi hatoshiriki kwenye fainali ya "American Idol" kutokana na kutopata kura za kutosha kumfanya aendelee.
Kijana huyo mwenye (20)sauti ya aina yake kutoka Westlake, La., jana aliondolewa katika mashindano hayo kwa kupata kura chache za watazamaji na hivyo kuwaacha Phillip Phillips (21) wa Leesburg, Ga., na diva mwenye miaka 16 Jessica Sanchez wa San Diego kuwania zawadi ya record deal katika fainali ya wiki ijayo.
Ledet alikuwa kipenzi cha majaji wote na mara nyingi wamekuwa wakisimama kumpigia makofi kwa jinsi alivyokuwa akiimba kwa ustadi mkubwa hasa alipowahi kuimba nyimbo kama "It's a Man's Man's Man's World" wa James Brown na "Runaway Baby” wa Bruno Mars. Hata hivyo uwezo wake huo haukutosha kushawishi kura za watazamaji.
Mtangazaji wa show hiyo Ryan Seacrest alisema jumla ya kura za watazamaji milioni 90 zimepigwa wiki hii.
Jumanne ijayo Phillips na Sanchez watachuana na Jumatano mshindi kuvikwa taji lake.
Unaona sawa kwa Joshua kutolewa?
No comments:
Post a Comment