Monday, May 28, 2012

Diamond ashutumiwa kuipa kipaumbelea zaidi Clouds Fm




Wakati wapenzi wa muziki wa Tanzania wakiendelea kuijadili performance ya Diamond jana kwenye Big Brother Eviction day, kuna wengine waliozitafsiri shukrani zake kwa vyombo vya habari kama za kibaguzi.

Hiyo ni baada ya Diamond kutoa shukrani kwanza kwa Clouds FM kwa mchango wake kutokana na mafanikio aliyoyapata mpaka kufikia kupanda kwenye majukwa ya kimataifa.

Baada ya kuandika hivyo, mmoja wa watu wanaomfollow mwanamuziki huyo kwenye mtandao wa twitter akaandika “inamaana media zingine hazimpi support Diamond?”

Diamond akiwa Airport Johannesburg asubuhi ya leo akijiandaa kurudi Bongo

Ili kufafanua Diamond akaandika “nimetweet hiyo coz ni media inayotoa habari za Bigbrother Africa, usinukuu tofauti kuleta malumbano tafadhali.”


Naye mtangazaji wa radio hiyo, Hamisi Mandi ‏aka BDozen akafafanua kwa kuandika, “nafikiri hii itakua ni special thanks!!!”

Kuweka mambo sawa zaidi kuhusiana na utata huo Diamond ametawaka watu wasinukuu tweet zake vibaya ili kuleta malumbano na kuwaomba wawe positive daima!

Baada ya kuipa kipaumbele Clouds FM, ndipo Diamond akavikumbuka vyombe vingine vya habari,” shukrani kwa media zingine zotee from Tanzania, kwa kusaidia kazi za muziki wa watanzania, mbarikiwe.

Baada ya kuiwakilisha vyema Tanzania, Diamond anarejea leo nchini.

No comments:

Post a Comment