Tuesday, May 22, 2012

Rumours: Selena Gomez ampiga chini Justin Bieber kisa Rihanna!



Mtandao wa MediaTakeOut umeripoti kuwa zipo fununu mtaani kwamba  Justin Bieber na mpenzi wake wa siku nyingi Selena Gomez wameachana.

Mtandao huo umesema kwa mujibu wa story za mtaa ni kwamba Selena Gomez amempiga chini Justin, baada ya kusikia fununu kuwa Justin na Rihanna wamekuwa karibu sana, na Selena anahisi huenda wameshavunja amri ya sita.

Na fununu za ukaribu huo wa Rihanna-Beiber umemkera pia CHRIS BROWN kiasi cha kumfanya amtukane kwenye remix yake ya  Theraflu.

Mtandao huo umeendelea kuyaunganisha matukio yanayosupport fununu hizo kwa kudai kuwa Justin alihudhuria tuzo za BILLBOARD siku mbili zilizopita akiwa peke yake bila Selena kitu ambacho si kawaida.

























Ushahidi mwingine ni kuwa  Selena ameacha kumfollow Justin kwenye Twitter!!!

No comments:

Post a Comment