Friday, May 25, 2012

Eryne Epidu amshutumu Mike T kuwa anataka 'kumloga'


Eryne

Mabomu ya shutuma ‘heavy’ kutoka kwa Eryne Epidu kuelekea kwa Mike T mshirika wake wa zamani katika biashara ya muziki, hayaelekei kusimama 'no time soon', bali ndo yanazidi kushushwa.

Baada ya kumshutumu rapper huyo wa ‘kama’ kuwa alimchomea kwa watu wa uhamiaji na hivyo kurudishwa kwao Uganda, sasa Eryne anadai kuwa Mike amemwandalia 'kamati ya ufundi'.

Ni usiku wa kuamkia leo ambapo Eryne amemshushia Mike bomu hilo ambalo limezidi kumchafua.

“Usiku wa leo (May 24), Mike T amebeba watu wasiojulikana kawaleta nyumbani Kimara ati, waje kusearch nyumba yangu. Watu 6 wamekuja bila kibali cha polisi na wanajidai ni polisi,” ameandika Eryne.

Kulifanya bomu hilo kuwa baya zaidi ya ‘guruneti’ katika CV ya Mike T jamaa akaongeza,“walitaka kuweka madawa au unga. Bahati mbaya wamekuta watu wako steady (ngangari).”

Kama haitoshi akaachia jingine “I wish I knew people but I don't. Jealousy na kutosoma. Maana taarifa ninazopata kutoka Dar eti zina uchawii ndani yake. Shetani mbaya nyie, ameanza kumdhalilisha mshikaji hadharani kwa kumfanya kama mwehu. Ndugu zake walio msindikiza usiku wa leo wamesikika wanasema anarogwa akiwemo shangazi yake.”

Mike T
Wakati Eryne akiwa haoneshi dalili zozote za kunyamaza, Mike yeye leo ameendelea kujipa moyo kwa ujumbe na tweets kama hizi “Life is not about the people who act true to your face. It’s about the people who remain true BEHIND YOUR BACK ,Thanks Allah” na hii nyingine “Like shedracky,meshacky and abenego thrown in the fire but they never get burn!!!”

Na baadaye kidogo mida ya saa 11:00 hivi asubuhi (May 25) akaandika “For my Own MISTAKES I don't wanna drag my family into this coz I do everything for them (my son, my daughter n my wife) ,for anyone who thinks for one way or another NIMEMKOSEA kimawazo , kimaneno au kimatendo its time I've to APOLOGIZE , am sorry Watanzania Wenzangu”

Bila shaka Mike T yupo kwenye mtihani mgumu sana katika maisha yake. 

It’s just getting started.

No comments:

Post a Comment