Sunday, May 27, 2012

Hofu ya usalama yasababisha Lady Gaga kusitisha concert ya Indonesia




Management ya Lady Gaga leo jumapili imesema mwanamuziki huyo ameisitisha show yake ya Jakarta, Indonesia kuhofia usalama wake baada ya wanaharakati wa kiislam kudai kuwa uvaaji na uchezaji wake unaenda kinyume na dini ya kiislam.

Kama show hiyo ikifanyika kuna hofu kuwa Lady Gaga, crew yake na wahudhuriaji kudhurika, amesema Minola Sebayang, mwanasheria wa mapromoter.

"Huu ni ushauri kutoka kwa timu yake ya ulinzi na usalama. Hivyo kusitishwa kwa show hiyo umetokana na uamuzi uliochukuliwa na management yake” alisema Sebayang.

Mapema mwezi huu polisi wa Jakarta walipendekeza kuwa show ya Lady Gaga iliyokuwa imepangwa kufanyika June 3 isipewe kibali kwasababu za kiusalama.

Kufuatia hatua hiyo Diva huyo wa pop aliandika kwenye Twitter jana jumamosi "There is nothing Holy about hatred." (Hakuna utakatifu katika chuki).

Ripoti za magazeti zilidai kuwa zaidi ya tiketi 25,000 zilinunuliwa ndani ya masaa mawili baada ya tiketi hizo kuanza kuuzwa mwezi March.

Polisi walidai kuwa promoter hakutakiwa kuanza kuuza tiketi kabla ya kupata kibali.

No comments:

Post a Comment