Friday, May 25, 2012

Nonini, French Boy na Levis waachia wimbo kuadhimisha siku ya Afrika


Nonini

Wakati leo ikiwa ni siku ya Africa ambayo husherehekewa duniani kote kila mwaka tarehe 25,May, wanamuziki wa Kenya akiwemo Nonini na French Boy leo wameachia wimbo kuadhimisha siku hiyo.

Wimbo huo walioshirikishwa na msanii mpya aitwaye Levis unaitwa ‘Africa’ ambapo wameitumia siku hii kumtambulisha msanii huyo.

Afrika wenye vionjo vya nyimbo za Afrika Kusini utakufanya usimame hapo ulipokaa na kuanza kuufuta mdundo wake mkali.

French Boy
Dhumuni la maadhimisho hayo ya siku ya Afrika ni kuangalia mafanikio ya bara kiutamaduni na kiuchumu.

Usikilize ama kudownload hapa:

No comments:

Post a Comment