Saturday, May 19, 2012

BBA: Muda wa huzuni, Prezzo achana mistari kwa Goldie, wasichana wavua (very sexy)


Muda wa huzuni

Jana wanaijeria walipata pigo kubwa baada ya wawakilishi wao wawili Ola na Chris kuamua kujiondoa Big Brother kutokana na sababu za kiafya. Baada ya tangazo hilo, upande wa Downville kulitawaliwa na majonzi makubwa wakati Ola na Chris walipokuwa wakiwaaga wenzao. Vilio,simanzi na kwikwi vilisikika kutoka kwa washiriki wanaobaki.



Wasichana wa Downville na dance za kichokozi

Baada ya yote hayo maisha ndani ya Big Brother upande wa Downville yakarejea kama kawaida. Akinadada wakajikuta wanapageuza casino kwa dakika kadhaa. Kila mmoja akatamani kusaula nguo (strip) mbele ya camera! And it was really sexy! Wengine wakavua suruali zao wakabaki na chupi tu then wakaanza kushake their asses! Wow! What a sexy moment ukiangalia.



Prezzo amchania mashairi Goldie

Katika scene nyingine wanaonekana DKB, Prezzo (wakiwa na magwanda yao ya adhabu) , Barbz na Goldie wakipiga story.Mara Prezzo akaanza kuimba wimbo wake For sho For Shizzle aliomshirikisha Ulopa. Wakati anaimba Goldie akawa anamuitikia chorus. Prezzo akachana mashairi kadhaa ya wimbo huo. DKB anaonekana haujui wimbo huo hivyo akamuuliza kama ameutungia humo ndani ama vp! Prezzo akamwambia ni wimbo wa kitambo na tayari video yake imeshatoka.



Prezzo  na Goldie ukaribu waongezeka

Kwa upande wa Prezzo ameonekana kutulia baada ya adhabu yao na DKB kumalizika. Kama kawaida yeye na Goldie wakatafuta chemba nzuri wakaanza kupiga story. Prezzo anasikika akimwambia Goldie kuhusu namna uzuri ndani ya moyo wa mtu unavyoweza kumfanya awe mzuri kwa ujumla. 


Kwa namna mchezo unavyokwenda, uwezakano wa Prezzo kukaa kwa muda mrefu mjengoni ama hata kushinda unazidi kuongezeka. Kwanza ni kutokana na wanaijeria wawili kujiondoa kitu kinachopunguza ugumu kwake kushinda kwakuwa wanaijeria watabaki na mshiriki mmoja tu Goldie. Kingine ni ukaribu wake na Goldie kitu ambacho kitamfanya azikonge nyoyo za wanaijeria ambao wataanza kumchukulia kama shemeji yao.


No comments:

Post a Comment