Sunday, May 20, 2012

Cyrill kuendelea na uzinduzi wa documentary yake


Uzinduzi wa documentary ya rapper Cyrill Francisco uliokuwa umezuiwa na baraza la sanaa la taifa utafanyika leo katika Ukumbi wa New Maisha Club kama ilivyokuwa imepangwa.

Awali BASATA iliwaandikia barua kali wamiliki wa ukumbi wa New Maisha Club kwa kile lilichodai kumleta msanii kutoka Kenya (Cyrill ambaye ni mtanzania hata hivyo) bila kibali na hivyo kuuzuia uzinduzi wa documentary yake FROM DAY ONE.

Akiongea kwa simu na leotainment leo Cyrill aka Kamikaze amesema imemlazimu kuwasilisha nyaraka muhimu kwa baraza hilo kikiwemo cheti chake cha kuzalliwa.

Rapper huyo aliyezaliwa mjini Kiomboi, Iramba, Singida amesema anaamini  jambo hilo limetokana na hujuma ya watu.

Miongoni mwa wasanii watakaompa kampani kwenye uzinduzi wake ni pamoja na Roma, Cpwaa, Izzo B, Godzilla, Hemed na Jelly wa Rhymes.

No comments:

Post a Comment