Saturday, May 26, 2012

Raz B wa B2K asema Chris Brown na Bow Wow ni ‘mashoga’



Raz B
Member wa zamani wa kundi la B2K Raz B, ameandika kitabu ambacho kimezungumzia uchafu wote uliopo kwenye muziki wa Marekani.

Kitabu hicho kiitwacho This Boy’s Life kimechapishwa na Corona Sky Production.

Kabla ya kufikia hatua ya kukiandika kitabu hicho, Raz B alikuwa ameshawahi kuandika kwenye Twitter kuhusu ujio wa kitabu chake.


Raz B anajulikana kwa tabia yake ya kuongea mambo mazito na hivi ndivyo alivyoandika:

Kuhusu Bow Wow:

Lil Fiz
“Bow Wow alikuwa mdogo kuliko sisi wote, lakini kampuni ilifikiria kuwa yeye kuwa karibu na (B2K) lingekuwa jambo zuri. Sikuona mwenyewe lakini niliambiwa na Fizz kuwa yeye na Bow Wow walikuwa na uhusiano. Sikufuatilia sana kipindi hicho. Baada ya muda ndo nikaja kugundua kuwa Fizz hakuwa anadanganya. Mwaka 2005 tena Bow Wow na Omarion wakawa hawatenganishwi. Baada ya kuwepo fununu kuhusu uhusiano wao Bow Wow aliamua kusitisha uhusiano. Story za ushoga zilikuwa zikiharibu biashara ya Bow Wow.”

Kuhusu Chris Brown:

“Wanasema huwezi kujua nani anamjua nani. Chris Brown hakufikiria hilo aliponishambulia online. Nina rafiki ambaye yupo karibu sana na kambi ya Chris ambaye aliniambia kuwa Chris alikuwa na uhusiano na mwandishi chipukizi wa muziki  Andre Merritt." 

Chris Brown
"Hivyo Chris alipoanza kuwaita watu ‘gay’ na ‘fags’ nikalitaja tu jina la Andre Merritt. Nilijua ilikuwa kweli pale alipouziba mdomo wake.”

Andre Merritt

No comments:

Post a Comment