Thursday, May 24, 2012

Updated! Diva wa Clouds FM kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake!



Bila shaka kupita hapa Leotainment umepata taarifa kuwa mtangazaji wa Clouds FM Loveness aka Diva anatarajia kujaribu bahati yake kwenye muziki wa Bongo Flava kuona upande huo wananchi watampokeaje.


Updates za story hii ni kuwa Diva huyo atamshirikisha pia Diamond kwenye wimbo utakaotengenezwa na Lamar.


Taarifa hizo zimethibitishwa na Diamond mwenyewe kupitia twitter ambapo alikuwa akimjibu mtangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV za Kenya, Willy Tuva "Kuna kibao nitafanya na Diva wa Clouds chini ya Fish crab cookout"

Diva ambaye hujiita ‘Mimi’ ni miongoni mwa watangazaji wanaozungumzwa zaidi nchini kwa mabaya  mengi na mazuri machache kutokana na aina ya utangazaji wake kwenye kipindi cha Ala za roho katika kituo hicho cha radio maarufu kwa burudani nchini kutokana na sifa yake ya kuongea mambo mazito ya kimapenzi bila kificho.


Diva anategemea kuachia wimbo utakaojulikana kwa jina la ‘Piga Simu’ chini ya producer Lamar wa Fish Crub!

Leo (May 24) Lamar ametweet “Diva aka mimi under xclusive muzik the lebal !soon to release a hit song piga simu.”


Yetu masikio kujua kama Diva atajikusanyia mashabiki pia katika muziki baada ya kufanya vizuri upande wa radio ama atawatukana tena wanaume! 


Mtangazaji huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kusema kwenye kipindi chake kuwa wanaume wa kitanzania ni wachafu,wananuka boxer,midomo,vikwapa n.k.

Unadhani Diva anaweza kuwa mwanamuziki mzuri?

No comments:

Post a Comment