Jay-Z amepanga kupumzika kidogo na muziki ili kuwa karibu na mwanae.
Rapper huyo mwenye miaka 42, amesema mwanzoni alikuwa amepanga kuingia studio baada ya kuzaliwa kwa mwanae Blue Ivy kwasababu kuzaliwa kwake kungempa mengi ya kuzungumza kwenye albam yake ijayo.
Hata hivyo, mpango huo sasa haupo tena.
"Nilidhani ningeweza baada ya mwanangu kuzaliwa. Nilidhani ningekuwa inspired zaidi kwa zile hisia mpya na kila kitu ambacho ningeandika, lakini imekuwa vingine” Hov aliiambia MTV News. "Nahitaji sana kuwa naye. Nataka sana kufurahia muda huo na yeye na nina uhakika hisia ile ya muziki itarudi tena”
Kwa sasa rapper huyo yuko busy na matukio mbalimbali. Pamoja na ziara ya barani Ulaya alioianza jana, ametangaza hivi karibuni kuwa ana mpango wa kufanya tamasha la muziki la siku mbili huko Philadelphia.
Atakuwa akiperform pia concerts kadhaa kusaidia kutangaza kufunguliwa kwa vituo vya Barclays huko Brooklyn alikokulia mwezi September.
No comments:
Post a Comment