Friday, May 25, 2012

C-Sir aamua kula boga na ua lake!



Katika maisha, hakuna kitu muhimu kama upendo. Kosa vyote lakini kitu hicho uwe nacho na wewe pia ukipokee kutoka kwa wengine.

Kwanini sasa tuwabague wengine kwa kasoro ama mapungufu yao na kuwanyima upendo? Wote kuanzia kipofu, kiziwi na walemavu wengine nao pia wanahitaji kupendwa na hatimaye kuoa ama kuolewa!

Hata wale walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi wanastahili kitu hiki cha thamani maishani.

C-Sir aka Madini haoni tabu kumpenda binti aliyeathirika kwa ugonjwa huo. Baada ya kugundua hilo hakupunguza mapenzi yake na amemuahidi kumpenda daima dawamu!

Msikilize hapo chini jinsi anavyosimulia kisa hiki ambacho ni utunzi tu kwake lakini kwa hakika wapo waliokutana na kitu hiki ambapo kuna wale waliochukua uamuzi kama wa C-Sir na wapo wale waliochukua uamuzi uumizao kwa kuwaacha wapenzi wao kutokana na kuathirika. Enjoy!

No comments:

Post a Comment