Wednesday, May 30, 2012

Dancer wa Nicki Minaj adaiwa kumbaka na kumuua shabiki


Nicki Minaj ameshtushwa na habari za kuuawa kwa shabiki yake nchini Japan.

Kupitia Twitter, leo Nicki ameandika, “Nimehuzunika baada ya kujua kuwa shabiki wangu wa thamani; amepatikana akiwa ameuawa nchini Japan. Upendo na sala ziende kwa familia ya Nicola Furlong.

Nicola
Imedaiwa kuwa Nicole aliuawa baada ya kubakwa na dancer wa Nicki Minaj James Black Stone aka King Tight pamoja na kijana mwingine.

Msichana huyo raia wa Ireland alikuwa nchini Japan kimasomo

No comments:

Post a Comment