Thursday, May 24, 2012

Ripota aliyembusu Will Smith aomba radhi


Vitalii Sediuk
Mwandishi wa habari wa Ukraine aliyejaribu kumbusu Will Smith alipokuwa kwenye uzinduzi wa filamu ya 'Men In Black 3' mjini Moscow wiki iliyopita, ameomba radhi kwa kitendo hicho.

Mwandishi huyo aitwaye Vitalii Sediuk na ambaye anajulikana kwa mchezo wake wa kubusu watu maarufu alijikuta akitandikwa kibao na Will aliyechukizwa na jaribio lake la kumbusu mdomoni.


Akiongea na Hip Hollywood, Sediuk amesema "Naomba msamaha kutokana na tabia yangu. Nadhani nilipitiliza.”


Aliongeza, "Will Smith ni mtu ninayemheshimu sana kama muigizaji. Nilipokutana naye Moscow, nilitaka kufanya kitu ili kumfurahisha."

"Tuna tamaduni za kislavic,” Sediuk anaendelea. "Huwa simbusu kila mwanaume ama mwanamke ninapokutana nao mtaani lakini muda huo nilitaka kufanya hivyo.”

Aliongeza "Siku nyingine nikikutana naye, nitashikana naye mkono tu.



No comments:

Post a Comment