Chris Brown ameshutumiwa kwa kuwahonga waandaji wa Grammy awards ili ashinde tuzo.
Mwanamuziki huyo wa 'Turn Up The Music' alisababisha gumzo mwezi February mwaka huu kwa si tu kuperform kwenye show hizo tangu apigwe marafuku miaka mitatu iliyopita kwa kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna, bali pia alipata tuzo katika kipengele cha Best R&B Album kwa albam yake F.A.M.E.
Chris Brown akishukuru kupokea tuzo ya Grammy Feb,2012 |
Hata hivyo imegundulika kuwa Chris aliwasumbua sana waandaaji wa tuzo hizo kwa kuwaandikia email kibao kuwabembeleza wampe tuzo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Inquisitr.com, Ken Erlich, ambaye ni producer wa zamani wa Grammy, Chris aliomba awahonge hela ili ashinde tuzo.
Huenda ikawa kweli kwakuwa Erlich alifukuzwa kazi baada ya tuzo hizo kwa kosa la kukiuka maadili na kuchafua heshima ya tuzo hizo.
Muda mfupi baada ya producer huyo kutimuliwa, rais wa The National Academy of Recording Arts and Sciences Neil Portnow, alitoa maelezo yasemayo:
Neil Portnow |
"Kwa takriban miaka kumi ya kuwa rais wa Academy, sikuweza kutabiri kama hili lingetokea. Msimamo wangu wa kutokubariki kutajwa kwa Chris kuwania tuzo hizi ulikuwa unajulikana.
"Nimefanya kazi na Ken kwa miaka sasa, na nimefedheheshwa sana. Nahitaji kurudisha uaminifu kwenye bodi hii na hamtaona kitu kama hiki kikitokea tena.”
Hata hivyo wasemaje wa Chris wamekanusha ripoti hizo na kuziita uzushi.
No comments:
Post a Comment