Tuesday, May 22, 2012

Wimbo wa mwisho kurekodiwa na Whitney Houston waachiwa



Ni miezi minne sasa tangu Whitney Houston afariki dunia lakini sauti yake inaendelea kuishi katika muziki.

Kabla ya kifo chake, Whitney alikuwa akishiriki kwenye filamu mpya akiwa na mshindi wa American Idol  Jordin Sparks.

Katika filamu hiyo iitwayo Sparkle,Whitney ameigiza kama mama wa watoto watatu wa kike ambao wanaanzisha kundi la kuimba na kisha kukabiliwa na changamoto za umaarufu na uraibu (addiction) wa madawa ya kulevya.

Kwenye movie hiyo Whitney amegiza kama mama mzazi wa Jordin Sparks.

Jana (May 21st) single ya kwanza kutoka kwenye soundtrack ya Sparkle imetoka.

Wimbo huo uitwao “Celebrate” ni wimbo wa mwisho kuwahi kurekodiwa na mwanamuziki huyo na umeandikwa na R Kelly huku Jordin Sparks naye akishirikishwa. Usikilize hapo chini.


No comments:

Post a Comment