Thursday, May 24, 2012

EXCLUSIVE: Nisher producer/msanii mwenye studio yenye thamani ya zaidi ya TZS mil. 150!



Nisher ni msanii na producer ambaye makazi yake ni jijini Arusha. 

Bado hajafahamika sana nchini lakini uwezo wake na muonekano wake ni wa kimataifa. Kuna vingi vinavyovutia kutoka kwake. 

Ukianzia na mwenekano wake ambao unaweza kukufanya udhanie ni mmarekani kama ukikutana naye.

Kingine ni kuwa mmiliki wa studio yenye gharama zaidi pengine kuliko studio yoyote ile nchini.

Katika mahojiano naye Leotainment imetaka kujua mengi zaidi kuhusiana na Nisher ambaye ni mtoto wa mhubiri maarufu nchini, GeorDavie, hasa kuhusu thamani ya studio yake.

Leotainment: Katika studio kali Tanzania yako imo aisee, thamani ya studio yako inaweza kufika ngapi?

Nisher: Vyombo havikununuliwa kwa siku moja. Ni mkusanyiko wa manunuzi toka mwaka 2005 hadi leo maana mwaka huo nilikua Marekani na miaka iliyofuata nikaenda nchi nyinginezo kama Holland, Dubai, Israel, Egypt na South Africa kimasomo, kimatembezi na kitalii.

Huko Huko nikaweza kununua vifaa vingi sana tena kwa Bei nzuri. Vinginevyo ni baba alinisupport kama kuwekeza katika kipaji/ujuzi/sanaa nilizonazo maana ni nyingi kwa kweli. Sasa ukichanganya na matengenezo ya studio (taa, fabrics, materials n.k mpaka hapo ilipo kwa haraka haraka thamani ya studio ni kama zaidi $100,000$ (zaidi ya shilingi milioni 150).Ila vitu vyote havikupatikana kwa siku moja.  Ni mkusanyiko wa manunuzi toka mwaka 2005 mpaka kesho.

Nisher Recors (Arusha)
Leotainment:Ulipokuwa nje ulipata uwezo  wa kuvinunua?

Nisher: Nilipokua nchi za nje nilikua nasoma lakini pia nilikua nikifanya kazi (Graphic Designes na Video & Music Production so hela niliyoipata nilikua
Pia Mara nyingi my dad Geordavie (Mchungaji/Mhubiri) ameamini sana katika talents zangu na ujuzi nilionao maana yeye ndiye aliyenifundisha kazi hizi mwanzoni. Kwahiyo amekua akinisupport kwa kiwango kikubwa zaidi.

Leotainment:Zaidi ya kuwa muimbaji na producer wewe pia ni director wa video, unajigawa vipi na huwa unalala saa ngapi?

Nisher: Dah! hapo ni pagumu japo nakuaga na ratiba katika kila ninachofanya (Work Plan). Rafiki yangu/Manager Addy John ( AJ ) amekua akinisaidia sana kuplan utendaji wangu wa kazi, kwamba wakati gani nifanye nini na wakati mwingine nifanye nini kutegemeana na mtiririko wa kazi kwa sababu nina kazi nyingi mno! Singer(Artist)/Song Writer/Composer/Graphics Designer/Music Producer/ Video Director & Editor/ Phototographer/ IT & web desiner nk . Lakini muda mwingi zaidi siku hizi nautumia studio kwaajili ya kujenga jina!

Kusema ukweli silali vya kutosha! Nafanya kazi masaa 18 kila siku, na wakati mwingine nakesha kwa masaa 72 (siku 3) bila kufunga jicho.
Marafiki zangu wa Facebook na Twitter ni Mashahidi maanake nakuaga napost vitu kibao kuhusu studio au kuhusu projects zangu nnline kwa masaa Mengi.
Wengine wananiaga wanalala na wanaamka wananikuta Bado nipo Online na napost! Energy (nguvu) yangu iko vizuri japo mama yangu (AnnaDavie) huwa ananiomba niwe na muda wa kupumzika angalau masaa 8 hadi 10.

Geordavie (Baba yake mzazi na Nisher
Leotainment:Kwanini ulifungua studio Arusha na sio Dar?

Nisher: Nilifungua studio Arusha kwasababu Arusha(ATL - Arusha-Town-Luxury) ndio mji wangu na ni mji wenye vipaji vingi vya kila aina lakini vichwa ( ma-producer ) vyenye International ideas ni vichache. Hilo ndo lililonisukuma kufungua studio Arusha.

Dar watu wengi tayari wana idea ya kufaya International Music ila basi tu hawafanyi kivile. Pia studios nzuri pia zipo Dar, nikaona kwanini tubanane wakati nina jiji langu hapa. Acha kwanza Nirepresent ATL to the fullest!

Leotainment: Una kipi kingine cha kuongeza?

Nisher: labda nitoe ombi tu kwa wadau wa muziki kwa ujumla na watanzania wenzangu kwamba, tusupport aina mbali mbali za muziki. Watu wengi kwa mfano wamesikiliza nyimbo zangu, wengi wamezikubali sana, lakini wengine wameniambia kwamba nisifanye sana muziki kama mbele yaani kama wenzetu (Ulaya, Marekani nk) bali ni jaribu kufanya zaidi mUziki usiwe mbali na nyumbani.


Lakini mimi nikajaribu kuwaza kitu kimoja, wadau/watanzania wangapi wanamfahamu Usher au watanzania wangapi wanamfahamu Chris Brown, watanzania wangapi wanamfahamu Jay-Z na kuskiliza nyimbo zao? Jibu lake ni wengi sana. Watanzania tunataka kufahamika nchi za wenzetu kwa aina mbali mbali ya muziki sio Bongo flava tu.

Inatakiwa wadau wa industry tanzania waone thamani ya kusupport aina ya miziki mingine kama R&B (ile ya ukweli sio bongo flavor), reggae, soul, jazz, country, charanga nk. Mbona  wameisupport hip hop Tanzania ikakubali? Sidhani kama kuna kitu kina shindikana duniani. Please Please wadau/ radio presenters/ djs na watanzania wote kwa ujumla huu ni mwaka 2012 bongo flava imechosha na inatosha! Watu tukae mkao wa kula aina ya muziki mpya na flava mpya kutoka kwa wasanii kama Nisher na wengine kibao.



Kama mtu anaweza kucheza akisikia track ya Rihanna kwanini asiweze kudance kwa beat ya Nisher na tena mimi bado nachanganya Kiswahili & Kingereza?  Tafakari. 

No comments:

Post a Comment