Monday, May 21, 2012

Mr Nice apewa shavu na ubalozi wa Mexico


Tangu producer Lamar amrudishe hewani na TABIA GANI Lucas Mkenda aka Mr Nice mambo yanazidi kumnyookea mhasisi huyo wa style iliyokufa ya TAKEU.

Wengi walikuwa wanaamini kuwa baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya miaka mitano mwanamuziki huyo asingeweza kurudi tena lakini mambo yamegeuka kuwa tofauti.

Na sasa akiwa tayari na albam yake mpya iitwayo TABIA GANI, Mr Nice amepewa ahadi nono na ubalozi wa Mexico nchini Tanzania kupromote albam yake. Hiyo ni baada ya kuyarudia mashairi ya wimbo uitwao El Rey ulioimba na msanii wa Mexico Jose Alfredo Jimenez.




Tafsiri ya mashairi ya wimbo huyo wenye maana ya mfalme yametafsiriwa na Dr Jose Arturo Saavedra Casco mhadhiri na mtafiti wa utamaduni wa Afrika na lugha ya Kiswahili katika kituo cha masomo ya bara la Asia na Afrika El colegio de Mexico.
Mr Nice katika ubalozi wa Mexico nchini
Katika wimbo huo Mr Nice anasikika akiimba style ya Ranchera maarufu nchini Mexico.


Wiki iliyopita msanii huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 35 aliutambulisha wimbo huo kwenye ubalozi wa Mexico nchini mbele ya balozi Mohamed Reza Saboor.

No comments:

Post a Comment