Thursday, May 31, 2012

Ngumu kuamini: Wanasema Beyonce ni mjamzito tena

Mtandao maarufu kwa kuibua mambo mazito kwenye masuala ya burudani, MediaTakeOut jana umethibitisha kutoka kwa snitch aliyekaribu sana na Beyonce kuwa mwanamuziki huyo ana ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Kwa mujibu wa mtandao huo story hizo si fununu, bali ni ukweli kabisa.

Umesema kwa mujibu wa snitch huyo aliye karibu naye, mama Blue Ivy hanywi tena pombe na ameanza kutumia vidonge vya FOLIC ACID. Vidonge vya Folic acid ni muhimu kwa akinamama wenye ujauzito mchanga.







Mtu huyo ameeleza, "Hakunywa kilevi chochote kwa wiki kadhaa na tuliagiza Petrus & Champagne mara kadhaa. Petrus ni wine aipendayo sana! Hakuwa yeye kabisa."



Mtandao huo umesema unategemea tangazo rasmi katikati ya mwaka huu pale ujauzito wake ukiwa mkubwa. Umesema sasa hivi una miezi miwili.

Kama habari hizi ni za kweli basi CONGRATS JAY AND BEY!!!

No comments:

Post a Comment