“Haya mapenzi yangekuwa kweli wali nisingeula, ningeuacha ulale ukiamka umechacha niumwage kabisa.” Ni maneno yanayosikika mwanzo kabisa kwenye Addicted.
Ni wimbo ambao unapoanza tu hivi lazima utajikuta kichwa chacho kinaanza kutikisika wakati mwingine bila wewe mwenyewe kujijua.
Hussein amekuja vizuri sana kwenye ngoma hii.
Ni ngoma yenye speed kubwa (120 bpm) unaofaa kuchezwa club. Tangu atoe full Shangwe iliyofanya vizuri kwenye club alijikita zaidi kwenye ngoma za kusikilizikad, na sasa muda aliokaa Kenya bila shaka umempa tution nzuri ya namna ya kutengeneza ‘club bangers’!
Huu ni wimbo ambao bila shaka unawakilisha ladha zote za Afrika Mashariki na kama ukipata promotion nzuri utampa show nyingi katika nchi hizo.
Ni wimbo mzuri kwaajili ya dedication kwa wale wanaopendana. Pia huu ni wimbo ambao unatoa jibu kuwa Machozi anafit vizuri kwenye muziki wa Kenya.
Ametuambia kuwa ameanza kulipa uzito wazo la kuhamia kabisa Kenya kwakuwa anaona mazingira ya muziki huko ni mazuri ukilinganisha na Tanzania ambako yeye anasema kumejaa unafiki.
Enjoy!
No comments:
Post a Comment