Wednesday, May 23, 2012

Ray J aruhusiwa kutoka hospitali



Baada ya juzi kulazwa hospitali Ray J ameruhusiwa kutoka na kufanyiwa uchunguzi kama mapafu yake yamevia damu sawa na ugonjwa uliomuua rapper  Heavy D.

Muimbaji huyo wa 'One Wish' alikimbizwa hospitali mjini Las Vegas jumatatu hii muda mfupi  baada ya tuzo za Billboard Music zilizofanyika usiku wa kuamkia siku hiyo.

Awali ilidaiwa kuwa Ray J alikuwa akitibiwa kutokana na uchovu baada ya kuwa na safari ya saa 32 kwenda China na kurudi na kisha kupitiliza Las Vegazi kuhudhuria tuzo hizo.

Madaktari walihofia kuwa Ray J anaweza kuwa na tatizo ambalo husababishwa na kusafiri kwa muda mrefu kwenye ndege.

Kwa sasa Ray J amerudi nyumbani Los Angeles kujiuguza zaidi.

Tunamwombea Ray J apone haraka!

No comments:

Post a Comment