Friday, May 18, 2012

Shambulio la 9/11 lilimpa kansa Donna Summer



Malkia wa Disco Donna Summer aliyefariki dunia jana kwa kansa anasemekana kuipata kutokana na vumbi lenye sumu lilitokana na shambulio la kigaidi la 9/11.

Mwanamuziki huyo wa The I Feel Love aliyefariki akiwa na miaka 63 kwa kansa ya mapafu, alikuwa mjini New York wakati Al-Qaeda walipoyashambulia majengo pacha ya Word Trade Center.



















Wakati ndege hizo zinagonga majengo hayo, yeye alikuwa kwenye nyumba (jengo) yake iliyopo karibu na hivyo kuvuta majivu yenye sumu yaliyokuwa na kemikali za asbestos, lead na mercury.

Yeye mwenyewe anasemekana kuamini kuwa kwa kuivuta hewa ile alipata kansa.



Inaaminika kuwa karibu watu 1,000 waliovuta hewa hiyo wameshakufa ambapo 350 kati yao ni kwa ugonjwa wa kansa.

No comments:

Post a Comment