Mesen Selekta |
Kwa wanaojua masuala ya muziki watakubaliana nasi kuwa vifaa vya gharama ama eneo la kupendeza iliyopo studio havimaanishi kuwa kazi zitakazotayarishwa hapo zitakuwa na ubora zaidi ama kufanya vizuri kwenye radio.
Cha kushangaza ni kwamba zipo studio zilizowekwa kwenye maeneo ya kawaida kabisa na zikiwa na vyombo vichache tu muhimu kama mic, mixer, kinanda, monitor speakers na vingine zina ngoma kali zinazotamba kila kona.
Pia zipo studio za ghali sana nchini lakini zinaweza zikapitisha mwaka bila kuwa na hit hata moja.
Utayarishaji wa muziki hutegemea zaidi kichwa na uwezo wa producer.
Producer mzuri anaweza kutengeneza hits hata kwenye studio zenye vifaa vya kawaida kabisa.
Producer mzuri anaweza kutengeneza hits hata kwenye studio zenye vifaa vya kawaida kabisa.
Na ndo maana watu wanashangaa studio inayokuja juu ya De Fatality chini producer mdogo Mesen Selekta inahit kinomanoma licha ya studio yake kuwa sebuleni! Yes sebuleni!
Msanii akiingiza vocal kwenye studio ya De Fatality |
Kila kitu kinapigwa sebuleni mwanangu! Ukija kusikia kazi iliyotengenezwa hapo huwezi kuamini zinavyosound poa!
Mesen amejizolea umaarufu mkubwa si tu nchini Tanzania bali hata Marekani kiasi cha kumfanya Dj Ill Will wa Marekani kutaka beat zake. Na sasa kijana huyu wa kitanzania amepewa assignment ya kutengeneza beat itakayomfit Chris Brown!
Mpaka sasa list ya wasanii waliofanya kazi na Mesen Selekta si kidogo kuanzia Solothang, Godzilla, Stamina, Ben Pol, Rich Mavocal, Mabeste na wengine kibao.
Mengi makubwa yanakuja kutoka kwa mchizi huyu.
No comments:
Post a Comment