Sunday, May 27, 2012

Vurugu kubwa zafanyika Zanzibar kupinga Muungano, magari yachomwa moto, watu wajeruhiwa


Vurugu ziliendelea hadi usiku

Kwa mujibu wa Radio One Stereo kumetokea vurugu kubwa visiwani Zanzibar baada ya kikundi cha Muamsho kuukataa Muungano.

FFU wakipambana na waandamanaji
Barabara zikiwa wazi kufuatia vurugu hizo
Katika vurugu hizo zilizotokea jana/usiku wa kuamkia leo kanisa na gari la Askofu limechomwa moto.

Mingoni mwa magari yaliyochomwa moto

Muamsho ni kikundi ya masheikh wa kizanzibar ambao mwanzo walikuwa wanahubiri dini kama mihadhara na sasa wamejiingiza kwenye masuala ya kisiasa.

Wanawake nao waliungana na wengine kuandamana
FFU wa Zanzibar katika jitihada za kuzuia maandamano hayo
Kufuatia maandamano hayo watu mbalimbali wa Tanzania bara na visiwani wapo kwenye mjadala mzito kupitia Twitter kuhusiana na tukio hilo na mustakali wa Muunguno.

@slimcony: “Wana uamsho wameanza muda mrefu, sasa wamepata nguvu, dai lao ni moja tu, hawawezi ungana na nchi ya kikafiri”

“Halafu wazanzibari walikuwa wanadai kitu simple sana.. Serikali 3, ya zanzibar, tanganyika na serikali kuu. Mmewanyima sasa wanaona bora muungano uvunjike”

‏@IdaHadjivayanis
It'll be naive for Tanzania to dismiss antiunion demonstrations as religious indoctrination- tangible action needed! #Zanzibar #Unguja

Ms. Issa ‏@Sashaissa
Ohhh #Zanzibar this is not the solution to our many problems...


KitaaOLOJIA ‏@FidQ
“Daang!Wanataka twende kwa viza sasa”

samira ‏@chibebi
“Mweh, Zanzibar jamaniiii mbona hivo....me rafiki yangu kaumizwa na kisu na gari yake imevunjwa vunjwa vioo kisa ina namba za huku bara!”

Maria Sarungi Tsehai ‏@MariaSTsehai
“mi binafsi nina marafiki zangu wazuri znz ambao hawautaki muungano - ni wasomi na akili zao timamu. Tusitake 'kupotezea' ishu hii kwa tukio”

“Naamini majority ya watanzania - bara na visiwani - hawapendi hawataki vita udini, tusikubali kuchonganishwa #ChangeTanzania.”

January Makamba ‏@JMakamba
“Lakini muhimu kutambua kwamba Wazanzibari wengi are tolerant. In fact Islam is a tolerant religion. Wachache wanaovuruga amani tusiwaruhusu.”

Aysha Mbarak ‏@3ashou
“My aunt's car got burned #Zanzibar #Unguja sad”

No comments:

Post a Comment