Friday, May 25, 2012

Unaijua page ya Facebook iitwayo ‘Tunakuchukia Diva’?



Hakuna mtangazaji wa radio hapa nchini anayejadiliwa kuliko Loveness aka Diva wa Clouds Fm.

Bahati mbaya hajadiliwi kwa mazuri. Hauwezi ukapita mwezi bila mtangazaji huyo wa vipindi usiku kuwakwazwa wasikilizaji kwa kuongea jambo fulani. 

Dada huyu ana utangazaji wa aina yake mwenyewe. Ni mtu asiyeogopa kuongea mtazamo wake hewani  ambao mara nyingi hupingwa na hivyo kumfanya ajadiliwe sana. 

Hivi karibuni amewaacha hoi watu baada ya kuwapa madongo wanaume wa Tanzania kuwa ni wachafu. Kauli hiyo imepokelewa kwa hasira kali na watu wa  jinsia zote ambao wanakielezea kitendo hicho kama ‘kuvuka mpaka’. 

Lakini Je! Unafahamu kwamba kwenye Facebook kuna ukurasa maalum uliofunguliwa na watu wanaomchukia Diva? Ukurasa huo wenye watu 2,610 unaitwa TUNAKUCHUKIA DIVA!


Hakuna kingine kinachoandikwa kwenye ukurasa huo zaidi ya matusi na madongo kwake.

“Yaani jinsi alivyokomaa anasema anamiaka 24 afu muongo fb kasema atasheherekea SERENA HOTEL kwenye kipindi anasema atasheherekea T.H.T diva bana yani wewe umbea wako,majungu yako,uwongo wako,ubaya wako,dharau zako,kuachika achika unaongoza,kutongoza wanaume kwakujigonga kwao unaongoza yani HUNA HATA HAIBA YAKIKE... UNAAIBISHA WANAWAKE WENZAKO WAKITANZANIA.....” Inasomeka miongoni mwa post mpya kwenye ukurasa huo.

Status nyingine inasema “Kesho ndo birthday ya dume jike DIVA ila najua anadanganya tuu kwajinsi alivyokomaa hana miaka 24 huyu.. so kesho mnataka page iweje tupost nini?????”

Na ijumaa hii, hiyo picha hapo chini ndiyo iliyowekwa kama status na watu wanachangia!


No comments:

Post a Comment