Tuesday, August 21, 2012

E-Newz (Channel 5) 21 August 2012

Bi Kidude anaumwa, mjukuu wake alalamika kuwa hana msaada



Taarifa kutoka Zanzibar zinadai kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Bi. Kidude anaumwa na hana msaada wowote.

Inadaiwa kuwa mjukuu wake alizungumza na televisheni ya Zanzibar na kulalamika kuwa bibi yake hana msaada na hivyo kumuuguza kwa shida.

Taarifa zaidi zinasema Bi. Kidude anaumwa tangu wiki iliyopita.

Where Have You Been ya Rihanna yafikisha views milioni 100+ ndani ya miezi minne



Rihanna ni mwanamuziki anayependwa zaidi pengine wa pili baada ya Beyonce duniani kama hatujakosea. Muziki wake umekuwa maarufu mno na bado anaendelea kufanya vizuri akiwa na miaka 24 tu. 

Mafanikio yake yamemfanya kuwa miongoni mwa wasanii matajiri zaidi walio na umri wa chini ya miaka 30.

Leo hii anasherehekea mafanikio mengine ya kuwa na video iliyoangaliwa zaidi Youtube ndani ya miezi michache. Where Have You Been iliyopo kwenye albam yake ya Talk That Talk imeangaliwa zaidi ya mara milioni 100 ndani ya miezi minne.