Kundi la Camp Mulla la Kenya Jumapili hii litakuwa live on stage katika Big Brother Eviction week.
Kundi hilo lilishindwa kuperform siku ya uzinduzi wa Big Brother Africa 7 ambapo wasanii waliopanda walikuwa pamoja na J. Cole, Davido, Aemo E'Face, P-Square, Naeto C na Flavour.
Ni kundi ambalo ukisikiliza nyimbo zake kama unaujua muziki lazima ujiulize kwa miaka mitano ijayo litakuwa wapi! Ni kundi pekee kabisa kuwahi kutokea Kenya ama hata Afrika Mashariki. Muziki wao ni wa town sana na kila kitu kwao ni unique!
Watu walianza kuziona cheche za Camp Mulla mwaka jana tarehe 12 February siku ambayo Collo aka king wa rap alikuwa ameandaa show ya Valentine na kuitambulisha ngoma yake mpya, Chini ya Maji.
Hapo hapo akalitambulisha kundi hilo kwa mara ya kwanza.
Mwezi huo huo nyota yao ikaanza kung’aa ambapo tarehe 26 wakafungua show ya P-Square katika ukumbi wa Carnivore. Baada ya hapo walipanda pia katika show iliyopewa jina Naija Nite ambapo Naeto C na Flavour walitumbuiza.
Kundi lenyewe linaundwa na vijana watano Taio Tripper ( Matthew Wakhungu) - Emcee, Rapper, vocalist, lyricist, Young Kass (Benoit Kanema) - Record producer, Rapper, songwriter, Miss Karun (Karungari Mungai) - Lead vocalist, songwriter, K'Cous (Marcus Kibukosya) - Record producer, MC, songwriter, rapper na Mykie Tuchi ( Michael Mutooni) – CEO.
Tunasubiri tuone jumapili hii watatokaje pale watakapokuwa wakiinadi style yao ya "2-5-Flow".
No comments:
Post a Comment