Tuesday, May 29, 2012

Hasheem Thabeet aja na kliniki ya kikapu June 1-2



Mchezaji wa Tanzania katika ligi ya kikapu ya Marekani, NBA Hasheem Thabeet ‏kwa ushirikiano wa Coca Cola Tanzania kupitia kinywaji cha Sprite ataongoza kliniki ya kikapu kwa vijana itakayofanyika kwa siku mbili nchini.

Kupitia Twitter Hasheem amesema, “Dar es salaam youth basketball clinic coming on your way starting on Thursday  when the kids from all over the country gets here!!!!”

Klinik hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam June 1 hadi June 2.

Hasheem na famili enzi za utoto wake
Katika hatua nyingine Hasheem anayechezea timu ya Portland Trail Blazers, amewaponda waandishi wa habari wasiofanya utafiti ama kwenda na mabadiliko ya technojia ya mawasiliano kwa kuuliza maswali yasiyo na msingi. “Haya maswali wanayouliza hawa jamaa kimtindo huwa hawafanyi research hata kidogo yaani dihh!! #waandishiwetu,” ametweet.

Hasheem ameongeza kwa kuandika kwa utani, “Mwandishi : Hasheem mbona umekuja kimya kimya?? me : ingia twirra ili usije uliza maswali ya kiduwanzi next time.. bwahahaha #waandishiwetu.”

Duu! kazi kwenu waandishi wa habari mlioachwa na wakati.

No comments:

Post a Comment