Monday, May 21, 2012

Mwanamke amvutia Fid amwandikie wimbo wa diss



Hivi karibuni katika session ya kila weekend ya kumuuliza maswali Fareed Kubanda aka Fid Q (#AskFidQ),aliulizwa amtaje msanii wa Bongo ambaye angependa amwandikie mashairi na yeye akamtaja Zavara pekee.

Well, inavyoonesha Zavara anaweza kupata mshindani aliyepigiwa passport ya kumwandikia mwana hip hop huyo na mwandishi wa mashairi mkali kuwahi kutokea nchini Tanzania.

Na tena kinachofurahisha ni kuwa mtu huyo ni mwanamke halafu angependa amwandikie trak ya kudiss! Fid kamjuaje na kwanini amemkubali?

“Daah.. Mitaa ya Kino nimekuta kuna mwanamke ana mchamba mwenzie hadi nimetamani kumuomba aniandikie diss track tatizo hana vina tu!!”

Tweet hiyo imewavutia wengi waliotaka kumjua zaidi mwanamke huyo. “Chukua tu mistari, vina utajaza mwenyewe (kicheko) Najaribu ku-imagine, ameandika mmoja wa followers wa Fid ambaye naye amejibu “Daah... Huyu shangingi simuwezi.

Mpaka kumshawishi Fid tunaamini mwanamke huyo atakuwa hodari sana katika sekta hiyo ya ‘uchambaji!

No comments:

Post a Comment