Sunday, May 20, 2012

BBA: Prezzo na Goldie ndani ya penzi zito



Inaonekana penzi kati ya Prezzo na Goldie linaendelea kushamiri.
Mchana wa jana mastaa hao walikuwa wamegandana kama gundi.
Muda wote walikuwa pamoja utadhani hakuna washiriki wengine ndani ya jumba hilo. Mara nyingi wameokana wakiwa kwenye kochi wakicheka , wakilaliana na kushikana mara kwa mara.

Roki alijaribu kuungana nao katika mazungumzo lakini wakampotezea hivyo kujiondokea na kutafuta jambo la kufanya na kuwaacha wapenzi hao kwenye mahaba mazito.



Barbz: Wananielewa vibaya

Katika hatua nyingine Barbz amekaa na DKB kuzungumza yaliyomo moyoni mwake kuhusiana na jinsi watu wanavyomuelewa vibaya na ndo maana akaamua kushiriki BBA ili watu wamfahamu vizuri lakini hata hivyo ndani ya jumba hilo bado wanamchukulia tofauti, jambo linalomuumiza sana.




Ni kubanjuka tu


Upande wa Upville baadaye pakageuka club ya disco. Ukapigwa muziki mtamu na washiriki wakasakata rhumba. Hata hivyo akinadada ndio waliojituma kucheza zaidi.

                  


Ukizingua, nazingua pia


Huko Downville mambo si mambo. Keagun(Afrika Kusini)  na Junia (Namibia) wakajikuta kwenye vita kali ya maneno.


No comments:

Post a Comment