Tuesday, May 22, 2012

Ray J alazwa hospitali kutokana na uchovu na stress


Siku mbili  baada ya tuzo za Billboard mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwanamuziki wa R&b Ray J amelazwa hospitali kufuatia ugomvi wake na wifi wa Whitney Houston katika tuzo hizo.

Imedaiwa kuwa Ray J alichukia baada ya ugomvi wa maneno kati yake na familia ya marehemu Whitney Houston uliotokea wakati wa tuzo hizo.

Asubuhi ya jana mtu wa karibu na msanii huyo alimkuta akiwa hoi kitandani na hawezi kuamka mwenyewe.

Baada ya kugombana na wifi yake na Whitney Pat Houston aliyedaiwa kumfukuza Ray J kwenye siti zilizokuwa karibu na wao, msanii huyo ambaye ni kaka yake na Brandy alizidiwa na kupelekwa hospitali na  ambulance.

Sababu za kupatwa na hali hiyo ni mchanganyiko wa uchovu na stress.

Kabla ya kuhudhuria tuzo hizo Ray J alikuwa amerejea kutoka China na alipofika Marekani, aliendesha gari kwa saa 4 hadi mjini Las Vegaz ambako tuzo hizo zilikuwa zikifanyika.

Kwa mujibu wa Pat , yeye alikuwa anamiliki tiketi sita za siti zilizokuwa mbele karibu na stage katika tuzo hizo. Waliokuwa wamekaa kwenye siti hizo ni pamoja na mtoto wa Whitney  Bobbi Kristina,  boyfriend wake Nick, rafiki yao na mbili zilikuwa wazi kusubiri wengine. 

Nick, Bobbi na Pat
Inadaiwa kuwa Ray J alitoka kwenye siti yake ya mwanzo na akataka kukaa karibu na Bobbi Kristina.

Wafanyakazi katika tuzo hizo walimwona Ray J akihama kutoka kwenye siti yake na wakamwomba arejee alikokuwa amekaa hata hivyo Ray J alikataa.

Wafanyakzi wa Hotel na walinzi walishuhudia msanii huyo akikataa kuondoka na hivyo nao kuingilia na kumuomba arudi kwenye siti yake. Baada ya kumwomba kwa muda mrefu bila mafanikio polisi wa Las Vegas ndipo waliitwa kumtoa Ray J.

Hata hivyo polisi walipofika, Pat aliwaambia kuwa yeye kama mmiliki wa siti hizo angemruhusu Ray J aketi.

Hivyo alikanusha maneno kuwa alimfukuza Ray J ambaye hata hivyo amesema “Pat aliharibu ile iliyokuwa fursa muhimu ya kumuenzi mwanamke niliyempenda”

No comments:

Post a Comment