Saturday, May 19, 2012

BASATA haijui kama Cyrill ni mtanzania, yazuia uzinduzi wa Documentary yake



Ama kweli vimbwega haviishi katika muziki wa Kibongo.

Ni ajabu kidogo baraza la sanaa la Taifa BASATA, lenye dhamana ya kusimamia sanaa ya taifa kumtambua Cyrill Francisco aka Kamikaze mzaliwa wa Kiomboi, Singida kama 'mkenya'.

Kitendo hicho kimesababisha katibu mtendaji wa BASATA Ghonche Materego kuwaandikia barua kali wamiliki wa ukumbi wa New Maisha Club kwa  kumleta msanii kutoka Kenya (Cyrill ambaye ni mtanzania hata hivyo) bila kibali na hivyo kuuzuia uzinduzi wa documentary yake FROM DAY ONE kesho (May 20).

“Katika vyombo vya habari umetangaza kumleta msanii Cyrill kutoka Kenya kufanya onesho tarehe 20/05/2012 bila kibali cha Serikali.

Huu ni ukiukwaji wa makusudi wa taratibu zilizowekwa na serikali na hivyo unaamriwa kusimamisha zoezi hilo na ueleze kwa maandishi kwanini usichukuliwe hatua za kishiria kwa ukiukwaji huo.

Maelezo yawe yamefika BASATA siyo zaidi ya tarehe 25/05/2012.” Inasema barua hiyo.

Gonche Materego (wa kwanza)

Akionesha mshangao  wa issue nzima Cyrill leo amesema  “eti wanasema NIMETENGENEZA skendo...huu ndio uthibitisho namba 1,namba 2 ni mazungumzo ya simu baina yangu na bosi wa BASATA leo mkuu Bwana LUHALA yaliyorekodiwa muda wowote ntayaweka hewani wananchi wenyewe mjaji tasnia yetu inapelekwa wapi. Eti wanasema mimi sio mbongo well wamepotea njia vibaya sana...#ILA WAJUE TU SHOW IPO KAMA KAWAIDA kesho pale Maisha Club Oysterbay..from WAKACHA ENT.

Jana msanii huyo aliandika "Inasikitisha kuona kwamba Tanzania bado kuna fitina za kurudishana nyuma kimaendeleo..sasa leo hii wanasema mimi sio mtanzania eti ni mkenya wakati basata jina langu lipo..sasa kama ni tecnic yao kunifelisha kwenye hii show wamepotea njia sababu,tarehe ni moja tu 20th may jumapili hii tukutane maisha club..ha ha ha ha. #WAMEOGOPA!


Je! suala la BASATA kumchukulia Cyrill kama msanii wa Kenya limetokana na uelewa mdogo wa BASATA juu ya wasanii wake ama ni Fitina ya mtu anayetaka kukwamisha uzinduzi wa Documentary yake? 

No comments:

Post a Comment