Monday, May 28, 2012

Bambo amshangaza Fid kwa 'kuichana' ielewe mitaa



Pata picha mchekeshaji matata, Bambo akichana mistari ya Fid Q aka Ngosha! 

Hata kama akipatia mashairi yote lakini version yake lazima iwe ya comedy na ni ngumu kujizuia kucheka akirap.

Hata hivyo Fid ameshangazwa na uwezo wa Bambo. Mchizi anaiweza Hip Hop!

“Daah.. Nimekutana na #Bambo Mlimani City halafu akaanza kunichania #ieleweMitaa #NimefurahiSana”, ameandika Fid.

Swali ni je! Muziki ulimshinda Bambo kiasi cha kukaa kimya tangu enzi za ngoma yake “Kitambi’? Ama kitambi kimeshamwelemea?



No comments:

Post a Comment