Thursday, May 31, 2012

Jessica Simpsons amuonesha mwanae Maxwell kwa mara ya kwanza

Hatimaye Jessica Simpsons amezionesha picha za binti yake kwa mara ya kwanza ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kujifungua.

Yeye na mwanae Maxwell Drew Johnson wameonekana kwenye cover ya jarida la People.

Akiwa amemshika Maxwell kwa mahaba mazito, Jessica anaonekana kujivunia na kuliambia jarida hilo kuwa mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Eric Johnson, amebadilisha maisha yake.



'Maisha yangu yamebadilika kabisa. Kuanzia jinsi ninavyolalala mpaka ninavyofikiria, Maxwell ametawala kila kitu!'

Aliongeza: 'Tunamtazama muda wote. Haturidhiki!'
 
Mwanamuziki huyo wa zamani aliyejifungua mtoto wake kwa upasuaji, ameliambia People kuwa kumlea binti yake ni kazi ya muda wote.


Mwanzoni iliripotiwa kuwa picha za Maxwell zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu, ziliuzwa kwa $800,000 kwa jarida hilo.

Hata hivyo kiasi hicho, ni kidogo sana kuliko walichowahi kupata mastaa wengine kwa watoto wao wa kwanza.

Jennifer Lopez alilipwa dola milioni 6 na jarida hilo la People kuonesha picha za wanae mapacha Max na Emme.

Jarida hilo hilo lilidaiwa kuwalipa Angelina Jolie na Brad Pitt karibu dola milioni 14 kuonesha picha za watoto wao mapacha Vivienne na Knox!

No comments:

Post a Comment