Wednesday, May 2, 2012

Mwanamke aliyezaa watoto wanane mapacha akubali kufanya video ya ngono

Unamkumbuka mwanamke huyu wa Marekani aliyejifungua watoto wanane mapacha,Nadya Suleman? Mambo yamekuwa magumu kutokana na kuwa na madeni yanayofikia £600,000 na sasa ameamua kucheza kwenye filamu ya ngono ili kujiokoa na mtihani huo!

Nadya, 36, alikuwa tayari mama wa watoto sita na kuzaa wengine wanane katika kipindi cha miaka mitatu tu na sasa ana watoto wanne wa kike na kumi wa kiume.

Sasa yuko mbioni kunyang’anywa mahala pa kuishi na pia anadaiwa hela na shule moja dini.

Mwaka huu tu Nadya alikubali kutokea kwenye gazeti akiwa kifua wazi na kulipwa £3,800 lakini aliapa kutoshiriki kwenye picha za ngono.

Video hiyo itaanza kuchukuliwa katikati ya mwaka huu.

"Kama ni kazi inayolipa na itanisaidia kuhamia kwenye nyumba salama ambayo nastahili, nitafanya" alisema Nadya.



No comments:

Post a Comment