Showing posts with label WORLD'S SHOWBIZ STORIES. Show all posts
Showing posts with label WORLD'S SHOWBIZ STORIES. Show all posts

Monday, August 20, 2012

Justin Bieber na Lady Gaga wamuunga mkono Beyonce kwa kampeni ya Humanitarian Day


Justin Bieber, Lady Gaga na Michelle Obama wamempa support Beyonce kwenye kampeni yake ya kimataifa ya World Humanitarian Day ambayo Beyonce aliiadhimisha kwa kuzindua video yake ya wimbo wake I Was Here, iliyochukuliwa wiki iliyopita kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Kampeni hiyo inawataka watu kuwasaidia wengine kama kupika chakula kwa wasiojiweza ama kutoa misaada.

Lengo ni kusambaza jumbe bilioni moja za matumaini.

Wengine wanaoshiriki ni Rihanna, Shakira, Jay-Z, Gwyneth Paltrow na Chris Martin.


Thursday, August 16, 2012

Flavour ashtakiwa kwa kucopy ‘Kwarikwa' kwa wasanii wa Ghana



Good news ni kuwa Flavour wa Nigeria ana hit mpya sasa hivi aliyomshirikisha Fally Ipupa iitwayo Kwarikwa ambapo sehemu ya video hiyo ilifanyika nchini Ufaransa. Bad news ni kwamba ngoma hiyo amecopy kwa wasanii wa Ghana ambao sasa wanadai chao.

Wasanii hao wa kundi la Wutah wanadai Flavour ambaye jina lake halisi ni  Chinedu Okoli ameiba utunzi wao.

Kwa mujibu wa vyanzo, wasanii hao Wutah Kobby na Wutah PV, wamesema hawajafurahishwa na tolea la wimbo huo uitwao 'Kwarikwa' ambao  unafanana na ngoma yao iitwayo Kotosa.

Wanamshutumu Flavour kwa kuiba chorus, rhythm,mashairi na saxophone iliyopo kwenye beat hiyo na kwamba wao ndio wamiliki halali wa vionjo hivyo.

Kotosa ulitoka mwaka 2008 kabla ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2010, na Kwarikwa ulitoka mwaka jana.

Hii si mara ya kwanza kwa Flavour kuiba vionjo vya wimbo mwingine kutoka nchini Ghana kwakuwa wimbo wake uliohit wa Nwa Baby ulikuwa na vionjo vya wimbo maarufu uitwao Ashawo uliokuwa maarufu nchini Ghana.


Koffi Olomide amtwanga mtayarishaji wake wa muziki



Mwanamuziki mkongwe wa Lingala nchini DRC Koffi Olomide anashitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.

Koffi alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani  jana baada ya kuzuka vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.

Inadaiwa kuwa kesi hiyo imevutia umati mkubwa wa watu mjini Kinshasa uliofurika mahakamani hapo kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.

Kesi hiyo iliharishwa hadi leo asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.

Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.

Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishaji wake Diego Lubaki, umetokana na kudaiana dola $3,680.

Kama akipatiakana na hatia Koffi anaweza kufungwa jela miezi sita.

Wednesday, August 15, 2012

Obama ana kiwanda cha bia ikulu!



Kuongoza nchi kubwa kama Marekani yataka moyo! Ndio maana Barack Obama aliamua kuwa na kiwanda cha bia kwenye ikulu ya White House ili kupunguza stress za cheo hicho kikubwa duniani. Isitoshe kipindi hiki ni kigumu kwake kwakuwa anaelekea kwenye uchaguzi, so kupiga mtungi si jambo la kushangaza kwake.


Amekuwa rais wa kwanza wa hivi karibuni nchini Marekani kunywa bia inayotengezwa kwenye Ikulu.


Bia inayotengenezwa humo imepewa jina la ‘White House Honey Ale’ ikiwa na rangi mbalimbali.

Asali kidogo inayopatikana kwenye bia hiyo inatoka kwenye mizinga ya nyuki anayofuga mkewe Michelle Obama kwenye bustani yao.

Picha: Beyonce atoa picha mpya za familia! Jay-Z mke anaye!

Bembea mtoto mzuri!
Michezo kama hii ni mbolea kwa ndoa yenye mafanikio
Jay-Z ndani na nje!
Wow!





Blue Ivy akipewa maziwa na mama yake

Tuesday, August 14, 2012

Wanamuziki 10 matajiri zaidi Afrika!

Youssou Ndour


1. Youssou Ndour

Huyu ndiye mwanamuziki tajiri zaidi barani Africa. Jamaa anamiliki kituo kikubwa zaidi binafsi cha runinga nchini Senegal, kampuni ya magazeti na kituo chaa radio.

Anamiliki pia night club na record label. Anamiliki kampuni ya nyumba na makazi. Mwaka 2004 jarida la Rolling Stone lilimwelezea kama mwanamuziki maarufu zaidi nchni Senegal na pengine Afrika aliye hai.

Tangu April 2012, ni waziri wa utalii na utamaduni nchini Senegal.

Matumizi ya nyimbo zake yanamuingiza mamia kwa maelfu ya Euro!


2.P-Square

Hakuna msanii wa kizazi cha leo anaeweza kugusa matawi ya mapacha hawa, Peter na Paul Okoye. Wana hela chafu!

Wanachaji dola 250,000 kwa kila show ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 390 za Tanzania! Kuongezea msumari zaidi hapo ni kwamba hawa jamaa wana show kila weekend! Mpaka sasa hivi wameshafanyiwa booking ya kufanya show sehemu mbalimbali duniani hadi March mwakani!

Nyumba yao waliyoipa jina la Squareville huko Ikeja Nigeria ina thamani ya dola milioni 3 ambazo ni zaidi  ya shilingi bilioni 4.

Waliweka historia kwa kuwa wasanii wa kwanza kununua kiwanja kwenye eneo la Banana Island nchini Nigeria ambacho kina thamani ya zaidi ya dola milioni 3 pia!

Wana mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya pili kwa ukubwa ya simu nchini Nigeria ya Globacom wakiwa kama mabalozi wake ambapo hulipwa dola milioni 1 kwa mwaka, wanamiliki pia mijengo kibao ya kupangisha.



3.D'banj

Mnigeria huyu aliye chini ya label ya Kanye West, G.O.O.D Music, alitengeneza takriban dola milioni 5 kwenye kampeni ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Anamiliki jina la ‘Koko’ linalojumuisha klabu bora za Nigeria za KokoLounge, maji ya kunywa Koko Water na Koko Mobile.

Aliwahi kufanya reality show ya TV  iitwayo Koko Mansion na kulipwa dola milioni 1.

Anamiliki nyumba yenye thamani ya dola milioni 1.5 jijini Atlanta. Ni mwenyekiti mtendaji wa Dbanj Records na pia ana kampuni ya ulinzi iliyofanikiwa sana.

Yeye hucharge dola 100,000 kwa show.

4.Koffi Olomide



Mfalme huyo wa Lingala anacharge tabriban Euro 100,000  kwa show. Jamaa hupiga show nchini Ufaransa zinazojaza karibu watu 80,000  ambapo tiketi moja ni Euro 30 sawa na shilingi elfu 60.

Amekwishatoa albam zaidi ya saba ambazo zimemuingizia mamilioni ya dola.

5.Salif Keita

Anajulikana pia kama ‘Sauti ya dhahabu ya Africa’, ni miogoni mwa watu wanyenyekevu lakini matajiri sana barani Afrika.

Msanii huyo albino anamiliki kisiwa chake binafsi nchini Mali.

Anamiliki majumba na mali zingine nchini Ufaransa na Mali.

6. Fally Ipupa

Msanii huyu anajulikana kama ‘Mfalme mpya wa Lingala’ wa DRC. Kutoka kuwa mcheza show wa zamani wa Koffi Olomide, anasifika kwa kuleta usasa zaidi kwenye muziki wa Lingala.

Ameshakuwa balozi wa brand nyingi za nguo nchini Ufaransa, concerts zenye gharama na kuuza kopi kibao za albam zake.


7.2 Face Idibia



Msanii huyu wa Nigeria anamiliki nyumba za kupangisha zenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.

Hulipwa kuanzia dola 50,000 - 80,000 kwa show.

Anamiliki pia klabu ya usiku ya nguvu na biashara zingine zinazomuingizia hela nyingi.

8.Hugh Masekela



Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa Jazz wanaoheshimika zaidi barani Africa.  Anamiliki mobile studio yenye mafanikio makubwa nchini Botswana. Hushiriki kwenye matamasha makubwa duniani na huingiza mamilioni ya dola kutokana na mauzo ya albam zake.

9. Banky W

Anajulikana kama Mr. Capable pia. Banky W hufanya show mara tatu ama nne kwa wiki zinazomuingiza mshiko mrefu mno. Aliwahi kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Estisalat ya Nigeria ambapo alitumika kwenye matangazo yake.

Kwa sasa ni balozi wa Samsung Mobile. Amewahi kufanya kampeni ya Coca Cola-Nigeria na Microsoft’s Anti-cyber Crime Initiative.

Kutokana na kuingiza hela nyingi amenzisha mradi kuwasaidia wasiojiweza kwa kuwalipia ada watoto wenye uwezo darasani chini ya Mr. Capable Foundation.

10.Chameleone

Mzee wa Valuvalu anafunga list kwa kuwa msanii mwenye hela zaidi kuliko wote Afrika Mashariki.

Anamiliki gari Cadillac Escalade yenye thamani kubwa, Mercedes Benz ML 320,  Super Custom, convertible na Premio.

Anaishi kwenye nyumba yenye gharama kwenye maeneo  ya wazito huko Seguku Hill kwenye viunga vya Kampala, simu zake mwenyewe na mali zingine nyingi.

Saturday, August 11, 2012

Jackie Chan kuwasili Kenya wiki ijayo

Jackie Chan

Muigizaji wa filamu Jackie Chan anadaiwa kuwa moingoni mwa watu mashuhuri kutoka nchini China watakaoitembelea Kenya wiki ijayo.

Atakuwa pamoja na mchezaji wa kikapu Yao Ming.
Yao Ming
Nyota hao wanaenda Kenya kushoot video ya kampeni kubwa itakayokuwa ikirushwa kwenye kituo cha runinga cha China.

Kampeni hiyo ni kwaajili ya kuzuia ununuaji wa pembe za ndovu na vifaru kutoka Kenya na kupelekwa nchini China kuuzwa.

Video: Rihanna alia kwenye mahojiano na Oprah kisa Chris Brown!



Oprah Winfrey anasifika kwa kuuliza maswali mazito na ya ndani. Wiki hii amefanya mahojiano na Rihanna aliyemfuata kwao Barbados.

Katika kipande kidogo cha  mahojiano hayo yatakayoruka August 19 kupitia kituo cha OWN,  Oprah alimuuliza kuhusiana na Chris Brown na jinsi alivyompiga, Rihanna aliyekuwa akitokwa na machozi alijibu “It was embarrassing. It was humiliating. I lost my best friend.”

Angalia kipande hicho kidogo.

The Expendables 2 kuingia sokoni August 17



Filamu ya Expendables 2 ambayo ni muondelezo ile ya mwaka 2010 inatarajia kuingia sokoni August 17.

Filamu hiyo imewahusisha waigizaji wakongwe, Sylvester Stallone kama Barney Ross ambaye ndiye kiongozi wa kundi la makomandoo wa The Expendables, Jason Statham kama Lee Christmas, ni mtaalam wa visu wa The Expendables, Jet Li kama Yin Yang, Dolph Lundgren kama Gunnar Jensen, Chuck Norris kama Booker, Jean-Claude Van Damme kama Jean Vilain (kiongozi wa upande wa maadui), Bruce Willis kama Mr. Church, Arnold Schwarzenegger kama Trench, Terry Crews kama Hale Caesar, Randy Couture kama Toll Road, na Liam Hemsworth kama Billy the Kid:


Bajeti yake ni dola milioni 100.

Baadhi ya waigizaji hao juzi Alhamis waliizindua filamu hiyo nchini Ufaransa na hizi ni baadhi ya picha za premier hiyo.

Van Damme akionesha kuwa bado anaweza  
Sly akiwa na Dolph
Kuanzia kushoto ni Van Damme, Arnord, Stallone, Jason na Dolph
Stallone na Arnord
Arnold, Stallone na Jason wakiteta jambo
Stallone na Jason kiuso wa mbuzi zaidi
Nani ana nguvu zaidi hapa?
Van Damme kazeeka siku hizi
Mnyama Dolph katika pozi
"Niko fit bado"

Thursday, August 9, 2012

Young Jeezy ateuliwa kuwa makamu wa rais Atlantic Records!


Rapper Jay Wayne Jenkins aka Young Jeezy ameteuliwa kuwa makamu wa rais wa  Atlantic Records.

Young Jeezy anaingia kwenye list ya rappers waliowahi kushika nyadhifa za juu katika label kubwa nchini Marekani.

Jay-Z aliwahi kuwa rais wa Def Jam, Jim Jones alifanya kazi kama makamu wa rais wa Koch Records, na The-Dream aliwahi kuwa rais wa Island Def Jam .

Jay-Z and Kanye West’s “Watch The Throne” Documentary (Video)



Now we all can see what it's like to work with Jay-Z & Kanye West!

Here is the never before seen documentary of the two rappers who rented a home in Paris to create the Watch The Throne album. Beyonce also makes a cameo in the video & we get an in depth look into Jay & Kanye's friendship & respect they have one another but above all else we get to see how they came up with the music! (HOT 97)

Wednesday, August 8, 2012

Jay-Z na Beyonce wanalipwa cash ndefu zaidi kuliko couple zingine za masupastaa



Beyoncé na Jay-Z hawana mpinzani kama couple maarufu kwenye hip-hop, lakini pia kwa mujibu wa jarida la Forbes wao ndo wanaolipwa hela nyingi zaidi kuliko mastaa wengine duniani walio kwenye ndoa.

Mwaka huu licha ya Beyoncé kuwa kimya kiasi kimuziki ameweza kuingiza diola milioni 40 na mume wake Hova, akiingiza dola milioni 38.

Kwa pamoja wameingiza dola milioni 78.

Wa pili ni Gisele na Tom walioingiza dola milioni 72.

Wengine waliongia kwenye list ni Posh Spice Victoria Beckham na mumewe mchezaji wa timu ya soka ya Los Angeles Galaxy David Beckham waliokamata nafasi ya 3 kwa kuingiza dola milioni 54.

Namba nne ni Brad Pitt na Angelina Jolie, wenye dola milioni 45.

Namba tano ni Will Smith na Jada Pinkett Smith walioingiza dola milioni 40.

Friday, August 3, 2012

Floyd Mayweather atoka jela




Bingwa wa ndondi nchini Marekani Floyd Mayweather ni mtu huru sasa hivi baada ya kuachiwa kutoka jela ya Las Vegas leo.


Mayweather aka Money alikuwa anatumikia kifungo cha miezi mitatu kwa kumshambuliwa mke wake.

Kutokana na kuonesha tabia njema gerezani bondia huyo ameachiwa mwezi mmoja kabla.

Boxer huyo alifuatwa na washkaji kibao kwenye gereza la ‘Clark County Detention Center’ akiwemo 50 Cent.



Binti yake mwenye miaka 12, Iyanna Mayweather na  meneja wake Leonard Ellerbe naye alikuwepo.

Thursday, August 2, 2012

Leona Lewis sasa kurap, amwambia Minaj: 'I'm coming for you Nicki!'



LEONA Lewis ameamua kujaribu bahati yake kwenye rap na albam yake mpya itakuwa imejaa michano tu.

Na mrembo huyo anajiamini kuwa atakuwa tishio kubwa kwa Nicki Minaj ambaye hana mpinzani kwa sasa kibiashara.

Mwanamuziki huyo wa Uingereza kwa sasa anamalizia malizia ngoma yake mpya ambayo anasema itakuwa tofauti kabisa.

Akiongea na gazeti la The Sun Leona amesema : "On my new album I will be rapping. I've discovered my voice for rapping.


"I could probably go up against Nicki Minaj now. I'm actually that good, so I'm coming for you Nicki! London style MCing."

Wednesday, August 1, 2012

Eddo wa Ebony Fm azungumzia sababu ya kumpiga msanii wa Iringa


Jana tuliandika habari kuhusiana na msanii wa Hip hop wa Iringa, Man Kichefu kudai kuwa amepigwa na mtangazaji wa Iringa Eddo Bashir. Leo tumezungumza kwa urefu na mtangazaji huyo kuchukua yale yaliyopo kwa upande wake.

Eddo amesema kilichotokea anakifananisha na kitendo cha mdogo kujaribu kumtukana mkubwa kwa makusudi ili  kumuona mkubwa atafanyaje.

“Yule mtoto kimuziki mimi nimekua naye, mimi ofcourse nilikuwa simjui lakini historicaly nimeambiwa kuwa kuna mtu mmoja anaitwa Meki ambaye kamdissi pia kwenye hiyo track.”

Anasema Meki ndiye aliyempeleka Man Kichefu kwa Amba (producer) ambaye alimfanyia wimbo bure iliyoitwa ‘Utanikumbuka’ ambapo Amba aliimba chorus.

“Ile track imekuja mikononi mwangu, nikaiona nzuri nikawa naipa airtime ya kutosha simjui na wala sijawahi kumtafuta,”anasema Eddo.

Kutokana na kitendo hicho Eddo anasema Man Kichefu alifanya jitihada za kumtafuta ili amshukuru kwa kumchezea ngoma yake hiyo.

“Mimi ndo mtu wa kwanza kumuita yule mtoto genious, na ana nyimbo zaidi ya tatu na nimempa interview zaidi ya saba,namfeel kwasababu anaweza kuandika.

Hakuna siku ambayo nimesema naomba kitu chochote kutoka kwake pamoja na support niliyokuwa nampa, lakini kwenye nyimbo anaimba, mimi naua muziki wa Iringa, mimi nachukua hela za wasanii kitu ambacho mimi nina watoto ambao wananifuatilia ninachokifanya na wanacatch vile ambavyo vimeimbwa mule.

Mimi nahangaika na muziki wa Iringa karibu nakuwa chizi na watu wanajua, hamna mtu ambaye hajapita kwenye mgongo wangu hata akifanya interview asahau kunishukuru. Piga story na Mike, Mike anatoka kwenye mgongo wangu, piga story na Squeezer, piga story na Dataz, piga story na Zay B,” Eddo aliongeza.

Mtangazaji na DJ huyo anasema baada ya kutopendezwa na kitendo cha Man Kichefu, aliamua kumuita studio ambapo hakukataa na kuanza kumkubusha alikomtoa. Hata hivyo anasema msanii huyo aliendelea kuonesha dharau kwa kumsukuma, kitendo kilichomuudhi.

“Kiukweli nilifanya kitu ambacho sikuwahi kukitegema kukifanya, kwasababu pia mimi ni binadamu wa kawaida, nilikuwa na jaziba. Kweli yule mtoto nimemchapa, sio kidogo, honestly na Mungu anisamehe, nimempiga sana yule mtoto … sana.”

Eddo pia amemshangaa Man Kichefu kwa kitendo chake cha kumdiss Amba kwenye wimbo huo wakati ni producer aliyemsaidia kwa mengi.

Hata hivyo amechukua nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki wake ambao hawajamwelewa kutokana na kitendo chake hicho cha kumpiga Man Kichefu.

Sikiliza interview yote hapa:

Kwa upande wa shutuma zilizotolewa na msanii hiyo kuwa Ebony Fm haitoi support kwa wasanii wa Iringa, mkurugenzi wa vipindi wa kituo hicho cha radio hiyo, Renatus Kiluvia aka Bizzo amekanusha kwa kudai kuwa hazina ukweli wowote.
Bizzo
Bizzo amesema Ebony Fm ina vipindi viwili vya muziki wa Bongo Flava ambapo kimoja ni kwaajili ya nyimbo zote kwa ujumla na kingine kikicheza nyimbo za wasanii wa eneo inaposikika redio hiyo katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Dodoma na Morogoro, Rukwa na Njombe.

“Tatizo ni kwamba watoto wa Iringa wanashindwa kutambua kwamba Ebony sasa hivi imetanuka, coverage imeongezeka.”


Msikilize zaidi Bizzo hapo chini