Wednesday, May 2, 2012

Profesa Jay na Solo Thang wachat kisiasa zaidi

Prof Jay
Unapowataja wasanii watano wa Bongo Flava ambao wamewahi kuandika nyimbo maarufu zinazozongumzia siasa na uongozi nchini Tanzania, Profesa J hawezi kukosa kwenye list.

Unakumbuka Ndio Mzee aliyompa shavu Juma Nature ilivyoshika enzi hizo? Huo ni wimbo ambao uliwakilisha hali inavyokuwa wakati wanasiasa wakijinadi kuomba kura za wananchi kwa kutoa ahadi kibao.

Kisha Prof J akaiendeleza story kwa kutoa “kikao cha dharura”. Wimbo huu ukaeleza namna mambo yanavyokuwa magumu kwa mwanasiasa mwenye ahadi za uongo ambaye hajatekeleza chochote katika yale aliyoyaahidi.

Kuumalizia muendeleo huo (sequel) akatoa Nang’atuka akimuelezea mwanasiasa huyu ambaye maji yamemkaba shingoni na hana jinsi zaidi ya kuachia madaraka.

Leo hii Profesa ametulia kidogo na kufanya ngoma zenye ujumbe tofauti na siasa lakini si kwamba haizungumzi siasa kabisa.

Leotainment imefuatilia mazungumzo yake na Msafiri Kondo aka Solothang katika mtandao wa twitter ambao wote kwa pamoja hawafurahishwi na mwenendo wa siasa nchini.

“Naona viongozi wetu hawana hata chembe ya huruma kwa wavuja jasho na wanaowapigia kura,naona laana ya dhambi inawatafuna sasa” aliandika Solo ambaye kwa sasa anaishi Dublin, Ireland kwa kumwelekezea Profesa J.
Solo 


Profesa alijibu “Huku ni vilio tu mzee tunapambana na mafisadi tu wanaogawana nchi yetu bila huruma wakati wananchi wanakufa na njaa!!”

“Yeah inatia moyo kuona raia wana mwamko wa kutosha kuhusu ufisadi sasa,mdogo mdogo mpaka tutafika tunapopataka,tumechoka sasa” Solothang.




Na kisha Mchawi wa rhymes akamalizia “We acha tu ndugu yangu ila wataisoma number maana wabongo wameshachoka kuburuzwa sasa kama MBWAI Basi MBWAI tuu”
Mazungumzo ya wasanii hao wawili wakongwe nchini Tanzania yamekuja katika kipindi ambacho baraza la mawaziri linatarajiwa kuvunjwa kutokana na miongoni mwa mawaziri kutakiwa kujiuzulu kufuatia kukithiri kwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma

No comments:

Post a Comment