Wednesday, May 2, 2012

MwanaFA na AY wanapanga kumrudisha GK?

Is this a little sign that they want to reincarnate the brother? Lakini katika case hii si kumfufua kutoka kwenye kifo bali kule alikokuwa amejificha.

Ni nani? Ni Gwamaka Kaihula aka King Crazy GK! Is he back in the game?

Picha yake akiwa na swahiba zake AY na MwanaFA imehit kwenye mitandao ya kijamii jumatano hii.

Kwa ufupi tu juu ya picha hiyo iliyowekwa Facebook na Hamis Mwinjuma aka MwanaFA kumesomeka
“With Ay & Crazy GK at Mjrecords... Stay Tuned”

Stay tuned kwa lugha yetu tamu ya Kiswahili inamaanisha “kaeni tayari". Kaeni tayari kwa lipi? Bila shaka kwa ngoma mpya tena pengine kutoka kwa mfalme huyu wa zamani wa East Coast Team!

Alikuwa wapi GK? Ni swali ambalo wengi wameliuliza baada ya kuiona picha hiyo.

“Duh GK mara ya mwisho nilimuona mwaka juzi maeneo ya Tambaza na mark II yake jamaa kajificha mno lol” ni comment ya miongoni mwa marafiki wa AY katika Facebook.

Mwingine aliuliza “AY wewe na Mwana FA mpo na mnatisha kwa sana tu yuko wapi GK?”

Kwa kifupi sana Ambwene akajibu “GK yupo, chuo kilimbana kiasi”

Ni jibu linalozua maswali mengi lakini angalau limetoa mwanga kuhusiana na ukimya wa mkongwe huyu wa muziki wa kizazi kipya Tanzania aliyetamba na vibao kama Miiko kumi ya rap, Sista sista na vingine.

Picha hiyo inatupa swali moja tu kubwa kuwa, ECT inarejea tena?


Picha na MxCarter

No comments:

Post a Comment