Wednesday, May 2, 2012

AY kufanya video itakayogharimu zaidi ya shilingi 31,740,000!


Miongoni mwa ‘qualities’ ambazo Ambwene Yessaya aka AY anazo ni kuwa mjasiriamali wa muziki na si mwanamuziki pekee kama wasanii wengi wa Tanzania walivyo.

Leotainment imethibitisha kuwa nguli (mogul) huyo wa muziki kutoka Tanzania anajiandaa kufanya video itakayomgharimu dola za marekani 20,000! 

Okay let’s do the math! kwa madafu shilingi ya Tanzania na kwa rate ya hivi karibuni ni karibu milioni 31,740,000, Duuuh!

Kibongobongo video yenye gharama saaana! kwa kuunganisha malipo ya Director/Producer,usafiri kwenda kwenye location, kulipia mavazi, kuwalipa watakaonekana kwenye video na mengineyo ni kama milioni tatu mpaka nne!

Kwa mkwanja huo atakaoukata, AY not only qualifies him to be a music mogul in Africa, he also deserves a head ‘honcho’ crown!

So issue iko hivi; Ngoma itakayofanyiwa video imetengenezwa na super producer Marco Chali wa MJ Records. AY amethibitisha kuwa video yenyewe itafanyika bondeni Afrika kusini mwezi huu.

Uchawi wote wa video hii utakuwa mikononi mwa kampuni iitwayo Godfather.

CV ya kampuni hii ipo vizuri kwakuwa tayari imeshapiga video kali za P Square na Mr Flavour wa Nigeria. Kwa mujibu wa AY quality za video za hawa jamaa haina tofauti na zile za Hollywood.





Hongera AY sifa kubwa uliyonayo ya kutake risk imekufisha hapo ulipo.

Usikose exlusive interview na AY hivi karibuni hapa hapa leotainment!

No comments:

Post a Comment