Showing posts with label BONGO CELEBS GOSSIP. Show all posts
Showing posts with label BONGO CELEBS GOSSIP. Show all posts

Thursday, August 16, 2012

Is Hussein Machozi single and ready to mingle?

'Shhhh! Usiniulize maswali mengi kama Polisi, wacha picha hapo chini iongee yenyewe'

Monday, August 6, 2012

“Nenda kwanza field”, Mpoki amchana Gossip Cop



Kwenye YOU HEARD ya XXL ya Clouds Fm, Soudy Brown amempigia simu Mpoki kumuuliza kuhusiana na story iliyoandikwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusiana na Masanja Mkandamizaji mwishoni mwa wiki iliyopita kudaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Katika mahojiano hayo Mpoki amemwambia Gossip Cop kuwa hana taarifa zozote kuwa Masanja amelazwa kutokana na kichapo hicho na kummshauri kuwa aende kwanza field ili ajifunze uandishi wa habari kwakuwa hauwezi.

Mpoki amejinadi kuwa yupo kwenye game kwa miaka 12 hivyo hayumbishwi na kitu.

Habari hiyo iliandikwa:

MCHEKESHAJI wa Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, mwishoni mwa wiki iliyopita anadaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea kwenye njiapanda ya Chalinze mkoani Pwani ambapo msanii huyo alikuwa akitokea Dar kuelekea Tanga huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu.

Chanzo hicho cha Ijumaa Wikenda kinachopiga kambi maeneo hayo kilieleza kuwa jamaa huyo alikutwa na kasheshe hilo baada ya ‘kuliovateki’ gari hilo lililokuwa likisindikizwa na polisi ambapo pamoja na kuzuiwa na wajeda hao, Masanja alijitoa fahamu na kujifanya kichwa ngumu.

Kilisema: “Baada ya ‘kuwaovateki’ wale polisi, ndipo nao (askari) wakamkimbiza hadi wakamkamata na alipotaka kuleta ‘mbovumbovu’ za kujifanya staa kama wale wenzake waliopoteza umaarufu na mvuto, ndipo akala mbata zake safi na soo likahamia kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze Njiapanda na kumshikilia kwa muda kisha kumuachia baada ya mahojiano.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Masanja ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kukamatwa na askari kutokana na makosa ya barabarani kwake ni suala la kawaida huku akikanusha kupewa kibano.

Wema na Diamond wanaumwa ugonjwa mmoja?

Wema Sepetu akichukua vipimo
Diamond alipokuwa hospitali baada ya kuugua ghafla
Pengine huu si muda wa kuendelea kuspeculate tena iwapo Wema Sepetu na Diamond wamerudiana. Kuna mambo mengi yanayoonesha dalili kuwa wapenzi hawa wa zamani wamerudiana. Hawajasema hadharani lakini picha za hivi karibuni zinaweka wazi. 

Kuanzia zile picha za Kigoma kwenye video ya Leka Dutigite na zingine. Lakini inaonekana kama vile Diamond na Wema Sepetu wanaumwa ugonjwa mmoja. 

Wiki iliyopita Diamond alionekana kwenye picha akiwa amelala kwenye kitanda cha wagonjwa na akichukuliwa vipimo na daktari. Na sasa kuna picha ya Wema akiwa kwenye kitanda hicho hicho na akichukuliwa vipimo vilevile kama Diamond. 

Daktari ni yule yule japo anaonekana akiwa na nguo tofauti. Swali ni je wapenzi hawa wanaumwa ugonjwa mmoja? Ama kuna kamchezo kaitwako 'Public Stunt' wanakacheza?

Friday, August 3, 2012

Hatimaye: Ray C kurejea Bongo


Baada ya kukaa nchini Kenya kwa muda mrefu hatimaye Rehema Chalamila aka ‘Kiuno bila mfupa, anatarajia kurudi nchini.

Taarifa hiyo imeandikwa na Sintah kwenye website yake ambaye tunahisi wamewasiliana.

“Jamani Rehema anarudi na this time kiuno kitazungushwa  kama feni ya nyumba ya kulala wageni chezeya yeye weweeee,hebu njoo shoga yangu ukonge nyoyo zetu,tulikumiss sana love, natamani ukifika tuu Airport unimbie ule wimbo nataka niwe na wewe milele,” , ameandika Sintah.

Hope habari hizo ni za kweli maana Sintah naye ana mambo mengi kama serikali.

Sunday, July 8, 2012

Nikki Mbishi amemdiss One The Incredible?



Okay, tunafahamu kuwa Nikki Mbishi na One The Incredible ni watoto waliokuzwa na baba mmoja kimuziki (MLAB Studio) chini ya producer Duke Touchez.

Mara nyingi wamekuwa wakifanya ngoma pamoja. Lakini kitu kimoja tu ambacho Nikki hakifurahii kila asikiapo jina la One! Ni kwamba wasanii wengi sasa hivi wanamuiga sana One katika uandishi na flow.

“EMCEES wengi wanataka kurap kama ONE The Inkredibo,hawajui kuwa Maalim Nash a.ka.Nash Mcee pia ni mcee mwenye mitindo hatari na hawajifunzi kupitia kwake#WAMEENEA KWENYE BOX NDO MAANA HAWAWEZI KUFIKIRI NJE YA BOX#,” ameandika leo jumapili kupitia Facebook.


Maalim Nash (kulia), mshikaji na Nikki Mbishi

Kwanini tunauliza kama Nikki amemdiss One The Incredible? Okay kama ulikuwa hujui ni kuwa kipindi Nikki Mbishi anatoka, alikuja na style yake ya kipekee ya uandishi na mituo kwenye vina vyake. Kwa muda mfupi sana style hiyo ikawaambukiza wasanii wengi wachanga. Kila mmoja akaanza kuandika na kutua kwenye vina kama yeye. 


Nikki, Stereo, One na washkaji

Kipindi hicho One alikuwa hajulikani kabisa. One amekuja kujulikana kwenye ngoma waliyofanya yeye,  Nikki,Godzilla na kumshirikisha Belle 9 kwenye chorus,’Kila Siku’. Hapo ndipo akagundulika msanii mwingine hatari kutoka MLAB!

One alipoachia debut single yake iliyoitwa The Incredible ndipo wakampa salute zaidi na hata kutishia crown ya Nikki Mbishi. Hata hivyo ukweli ni kwamba One aliwahi kukiri kuwa anamuogopa sana Nikki Mbishi kwa uandishi!

Then tunapoona status kama hiyo iliyoandikwa na Nikki hasa kwa kumsifia Nash mc dhidi ya One, it sounds like a potential diss to us! Let’s wait.  

Tuesday, July 3, 2012

Wema Sepetu ni mjamzito?



So Wema Sepetu strikes again? This time sio kuhusu wedding dress tena na mipango ya harusi kama alivyosema last time. Sasa hivi kaja na jipya. We must admit that she is very good at teasing her followers on Twitter with controversial statements and unfortunately we all fall in her deliberate traps!

Okay weekend iliyopita kaja na jipya. “Am not in a good kabisa! hichi nachokihisi ndo chenyewe ama? Hehehhehhe,” alitweet.

Tafsiri ya haraka haraka kama ndo umekuta na sentensi hiyo mbele ni nini? Ofcourse, sisi pia tunafikiria hivyo hivyo unavyofikiria sasa, kwamba anahisi ni mjamzimto, what else?

Kama kawaida followers wake wakaingia kwenye mtego na maswali yakaanza, “Wema kipi tena?,” That’s what she wanted to hear right? “Shijuwiiiiiiii,” alijibu na kuchokoza maswali mengine yalioanza kumkera tena! “Hiyo ya Diamond au?,” akaulizwa na mtu mwingine, (Prank gone wrong Wema?). Hata hivyo alijikaza na kujibu, “Umetumwa?”

Baada ya kusikia Diamond kaingizwa kwenye mazungumzo akaamua kukaa kimya kama panya aonapo paka, na mada ikabadilika.

Katika hatua nyingine picha za hivi karibuni za Wema zinazomwonesha akiwa mweupe zaidi ya mwanzo, zimekuwa topic kwenye mitandao ya kijamii. Wengi wameoneshwa kutofurahishwa na mabadiliko hayo makubwa ya ngozi yake ambayo wanadai yametokana na mkorogo.

“Wema wa zamani alikuwa mzuri sana natural colour, kwa sasa hivi umekuwa una rangi mbaya ya ngozi.Naweza kusema inakaribia kufanana na ya Michael Jackson,” aliandika msichana mmoja aitwaye Mariam.

Msichana mwingine aitwaye Pauline alimtetea kwa kusema: “Hakuna aliyekamilika chini ya jua na siku zote embe tamu na lililoiva ndio linalotupiwa mawe.Kiukweli Wema ni mzuri ndio maana anafuatwafuatwa mara magazeti mara raia, hebu muacheni jamani mnamsema kwa mabaya tu ina maana huyo Wema hana jema hata moja?”

She looks beautiful though, doesn’t she?

Saturday, June 16, 2012

Fina Mango kwenda Radio One?


Tangu aache kazi Clouds Fm, watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali lini mtangazaji wa kike mwenye sauti nzuri pengine kuliko wote Tanzania (kwa mujibu wetu) Fina Mango atarudi tena hewani?

Kwa muda wote huo tangu aache kazi ya utangazaji amekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya 1Plus Communication ambayo hujihusisha na mambo PR na uandaaji wa matukio.

Leo hii tunaweza kukupatia clue kidogo ya future yake katika utangazaji kutokana na kile alichokiandika kupitia Twitter.

Tangu asubuhi Fina ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto wa kiume aitwaye Ben, amekuwa akiimwangia sifa Radio One kiasi cha kutupa maswali labda akatua hapo siku zijazo.

‘Kipindi cha watoto Radio One chanifurahisha. 'Kitendawili.... '

Akaongeza nyingine, “Dont say this a lot but nice music on Radio One.”

Mwisho akamalizia hii, “Aise seriously Kwa watu wazima Kama mie very nice music on 89.5FM Radio one with Abubakar Sadiq na DJ White. Sijui jina la show.” Sounds fishy right?


Tuliamua kumtwanga swali ili kusikia anasemaje, "Any plans kuongeza majeshi Radio One! I can c more and n mo compliments about the legend Radio Station today! They will be happy!! Naye akajibu, "haha walikua wanapiga nice old tunes that's all. Hamna zaidi."

Hivi karibuni Fina alifanya interview na mtandao wa ‘Bongo Celebrity’ na kuuambia kuwa fununu za kwamba anafungua radio station yake mwenyewe si za kweli japo hewani atarejea kwa nguvu mpya kwakuwa amewamiss sana pia wasikilizaji wake.

“Hapana sio radio yangu mwenyewe. Masoud yupo hewani tayari Times FM na ninatumaini kufanya mambo yangu kwingine pia….. Nipo kwenye maandalizi ya mwisho, so sooon!


Thursday, June 14, 2012

Hii remix ya Hold Yah ya Stanboi katisha aiseee!



Muda mfupi uliopita kupitia Twitter msanii wa Tanzania aishie Wichita, Kansas, Marekani Stanboi amesambaza remix yake ya wimbo maarufu sana wa Gyptian Hold Yah!

Ni wimbo mfupi sana haufiki hata dakika mbili lakini ukiuskiliza utatamani kama ukikutana naye umwambie aungeze uwe na hata dakika nne hivi.

Kama angeiitoa remix hii kipindi ambacho wimbo original ulikuwa hot tunaamini ungemfikisha mbali sana hasa kama angeusambaza sehemu kubwa.

Kwa wale waliokuwa na doubt naye huenda wakimsikiliza humu wanaweza kubadilisha mawazo yao.

Well done Stanboi aka The African Child

Tuesday, June 5, 2012

Diva: Nadhani utajiri wa waigizaji wa kike Bongo unatokana na kujiuza


“Seriously wasichana wa Bongo movies mnaweza kuwa mnaingiza pesa kiasi hicho cha kumiliki hizo gari za kifahari?! Don't buy this!!”

Hiyo ni kauli ya mtangazaji maarufu wa Clouds FM Loveness aka Diva ambaye anaungana na watu wengi wenye mashaka hayo ambapo kila mmoja anafikiria sababu yake mwenyewe kuhusiana na wapi actress wa Bongo wanapata hela ya kufanya waishi ‘Hollywood-like life.’

“I think kuna watu selling their dignity for money ......kabisa,” amezungumza Diva na kuweka wazi anachodhani ni chanzo cha maisha ya kifahari ndani ya Bongo movies.

Wengine kama ilivyozoeleka siku hizi hawakuchelewa kuhusisha na Freemasons.

“What do you think about them,freemason au?” Diva akatupiwa swali. Tofauti na wengi wanaodhani wanaweza kubashiri jibu la mtangazaji huyo, yeye amesema,”Freemason Tanzania kwa stars wa movie and music? Lmaoo ,never!!”

Msimamo wake umebaki pale pale, “Ningekuwa mwanaume ningeimba bado nipo nipo sana kama mwanafa.My dad is right, he said some of african girls trade sex for money,shame man.”



“How can u just go around and bang Everyone? Vagina gon get large and u gon catch Em STD's , I lov My life&believe inlove daily.”




Mjadala huo kuhusiana na utajiri wa kupindukia wa waigizaji wa kike wa filamu nchini uliongezewa mafuta zaidi hivi karibuni baada ya mtandao wa Global Publisher kutoa picha za magari yanayomilikiwa na Jackiline Wolper.

Mrembo huyo yuko fit haswaa kwani anamiliki gari aina ya BMW X6 lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170, Toyota Noah lenye thamani ya Shilingi milioni 18 na Toyota Harrier Lexus lenye thamani ya Shilingi milioni 25 ambalo linatumika kuwapeleka wadogo zake shuleni.

Kwa upande wake mtandao wa Dartalk, ulijaribu kufanya uchunguzi zaidi ili kuujua ukweli.
Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa na mtandao huo February mwaka huu, muigizaji huyo anatembea na kigogo wa benki kubwa Tanzania, ambaye familia yake inaishi nchini Marekani.

Uchunguzi wa mtandao huo ulibaini kuwa msanii huyo amekuwa akipewa shilingi milioni 3, kwa siku kwa ajili ya matumizi na kigogo huyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa DarTalk, Jackline alikanusha story hizo.










Picture Credits: Global Publishers

Shaa awapuuzia Uwazi kuhusu kuachana na Master J!




Katika hali inayoashiria kuwa mwanamuziki wa kike nchini Tanzania Sarah Kaisi aka Shaa ameipuzia habari ya gazeti la udaku la Uwazi kuwa wameachana na mpenzi wake wa zamani Master J, ameliscan na kuliweka Twitter.

Shaa
Gazeti hilo lililotoka leo (June 5) lina kichwa cha habari kisemacho "Master Jay & Shaa wamwagana. Babu Tale atajwa kuwa chanzo, Master Jay aelezea kilichotokea."

Akiwa amemkopi @masterjtz , Shaa ameandika “Woke up to this...cute! For show bookings,interviews and all plz contact Babu Tale.”

Master Jay
Gazeti la uwazi linasema wapenzi hao wameachana kisa Babu Tale. Hata hivyo Shaa ameendelea kusisitiza juu ya watu wanaotaka kufanya show naye wawasiliane na Tale ambaye inavyoonekana ni meneja wake.

Babu Tale
Wakati Master Jay yuko busy na EpiqBSS, snitches wako busy kuiangalia ‘Siri ya Penzi’ kati yake na Shaa. 

Habari hii inaweza kuwa ya kweli?

Thursday, May 24, 2012

Hussein Machozi akana kuwa na uhusiano na Avril (Kenya)


Hussein Machozi
Kuna story zinavuma nchini Kenya kuwa Mzee wa ‘Kafia Ghetto’ na ‘Full Shangwe” Hussein Machozi ana uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wanamuziki warembo kabisa Afrika Mashariki, Avril Nyambura!

Hata hivyo Hussein mwenyewe amekataa kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Wawili hao wamedaiwa kuwa na uhusiano baada ya kuonekana mjini Mombasa wakiwa karibu mno baada ya show waliyokuwa pamoja.

 “Avril ni rafiki yangu wa karibu kama msanii yeyote yule. Mimi niko single na muda wa mambo hayo utafika tu” Hussein ameiambia website ya The Star ya nchini Kenya.


Avril
Baada ya kusoma taarifa hiyo tumemuuliza pia Hussein kuhusiana na tetesi hizo ambaye amejibu "aaah hamna bana labda wameona tupo karibu tu wakaona namgonga bana..wala hakuna kitu na huyu mtoto.."

Katika hatua nyingine Machozi amerekodi wimbo uitwao 'Addicted' na mwanadada anayetamba sana kwa sasa nchini Kenya Size 8. 


Machozi anasema wimbo huo ni kwaajili ya mashabiki wake wa kike ambapo video ya wimbo huo itafanywa na kampuni ya Ogopa DJs ambao ndio walioutengeza wimbo huo.

Size 8
Mwanamuziki huyo kutoka Singida yupo nchini Kenya tangu kipindi cha pasaka na amekuwa akipiga show baada ya show.

Wednesday, May 23, 2012

Makala: AY na B’Hits na urafiki uliochuja kimya kimya



Kwa muda mrefu sana Hermy B, CEO wa B’Hits Music Group na Ambwene Yesaya aka AY walikuwa maswahiba zaidi ya chanda na pete. 
Uhusiano wao ulikuwa na mafanikio kwa kila mmoja. Nyimbo kama habari ndio hiyo, nangojea ageuke, Leo, Bed and Breakfast na nyingine nyingi zake AY zilitengenezwa ba Hermy B ambaye pia ni jaji wa mashindano ya Tusker Project Fame. 
Kabla ya nyimbo hizo ni wachache sana waliokuwa wanamjua Hermy B. Ni wazi kuwa AY alimtambulisha Hermy kama miongoni mwa watayarishaji wazuri nchini Tanzania.
Lakini hivi karibuni kumekuwepo na fununu kuwa ushkaji kati ya nguli hao umefikia tamati. Tweet hii iliyoulizwa kwa AY na mdau mkubwa wa leotainment @Haile19 leo (May 23) ikatupa jibu la maswali yetu kuhusiana na tetesi hizo “ni kweli ur not with #Bhitz anymore!” ambapo AY amejibu moja kwa moja “YES”
Mashaka kuhusiana na uhusiano wao yalianza kuonekana baada ya AY kuwa na mpango wa kwenda kufanya video nchini Afrika Kusini akiwa na producer wa Mj records, Marco Chali ambaye ndiye aliyeutengeneza wimbo huo. Na jana (May 22) wamewasili mjini Johannesburg kwa ajili ya shughuli hiyo.


Wakati wa urafiki kati ya AY na Hermy hakuna kazi ambayo AY alikuwa akiifanya nje ya usimamimizi wa Hermy. Uamuzi wake wa kwenda kufanya kazi MJ Records ukaashiria kuwa uhusiano wao umeingia matatani. Kuna maneno pia sababu za kuvunjika kwa ushkaji huo umetokana na tamaa ya Hermy B ambaye alidaiwa kumtaka AY aanze kumlipa producer huyo shilingi milioni 10 kwa wimbo mmoja.
Kwa wengi kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa Hermy alianza kuingiwa na kinyongo na kuona kuwa analipwa kiasi kidogo licha ya AY kufanya show nyingi ndani na nje ya nchi zinazomlipa sana. Kwa kawaida kama huo ni ukweli basi Hermy alikuwa sahihi kwamba kwanini umlipe laki 4 ama tano kwa single moja wakati wewe unaingiza zaidi ya milioni 20 kwa wiki moja ama mbili (makadirio).
Hata hivyo shilingi milioni kumi kama tozo ya wimbo mmoja kwa Tanzania bado haiwezi kuwaingia akilini wasanii wengi hata wale wenye kipato kikubwa akiwemo AY.
Sababu nyingine ya wazi kabisa kuwa AY na Hermy si ‘wana’ tena ni ukaribu wa hivi karibu kati yake na Master J ambao bila shaka umetokana na uswahiba wa Master J na Salama Jabir ambao nao ulitokana na kuwa majaji wa Bongo Star Search. Pamoja na kuwa Master J na AY wanafahamiana tangu siku nyingi kama msanii na producer, tunahisi kuwa ushirikiano wa AY na Salama Jabir katika kuanzisha kipindi cha TV cha Mkasi kimewaweka karibu zaidi Master J na AY kwa kupitia Salama.

Sababu ya tatu iliyotufanya tutilie shaka uhusiano wa B’Hits na AY, ni kile alichokisema Hermy B na kuandikwa hapa mwanzoni mwa mwezi huu kuwa hakuna msanii tajiri Tanzania.

Kauli hii ya Hermy ilitupa mashaka na kuiona kuwa huenda imetokana na kitu kinachomuumiza moyoni hususan mafanikio ya AY ambaye wengi tunaamini ni miongoni mwa wasanii matajiri nchini Tanzania.
Hata kama AY na Hermy B (B’Hits) wakiendelea kutokokuwa karibu kimuziki, walipofika wote si pa kubeza na kutokana na ubunifu, kujituma na uwezo wao binafsi kila mmoja ataendelea kupata mafanikio katika upande wake na maisha yanaendelea

Friday, May 18, 2012

Eryne: Nimelazimishwa kurudi Uganda na Mike T


Eryne, Witness na Fid Q
Hivi karibuni jina la Eryne Epidu lilitokea kuwa maarufu sana kwa kazi zake nzuri za video alizokuwa akizifanya katika kampuni ya Showbiz Defined iliyokuwa ikimilikiwa kwa ubia na yeye,  Mike T na Witness.

Baadaye kukawepo na taarifa kuwa Eryne ambaye ni raia wa Uganda amehamia kwenye kampuni nyingine tena.

Hiyo ikaashiria kuwa kulitokea kutoelewana kati ya mafahali hao wawili.

Katika kuwasiliana na Eryne kwa issue zingine kabisa tukagundua kuwa hayupo Tanzania na tayari yupo nchini mwao Uganda.

“Haya bwana nililazimishwa kuondoka ndugu yangu. Mike kaniletea mbwa hadi nikaona aina maana.” Aliandika Eryne.

Kuhusu kama ana mpango wa kurudi Tanzania kuendelea na kazi zake Eryne amesema “Am not planning to come any time soon. Mwaka huu kwangu bongo imekua sumu. So nahitaji kutulia nakufanya kazi na watu wazima kidogo.” Alisema.

“Ingawa ntamiss sana bongo. Miaka kumi hapo, lakini kila kitu kimekufa kwa tamaa ya mtu moja. Nasikia leo (May 17) RFA walitangaza kwamba katapeli (Mike T) hela show ya Bob Junior ya Kenya.”

Kauli hiyo ya Eryne ambaye pia aliwahi kuwa manager wa Witness, ikatuongezea scandal nyingine inayomwandama “mnyalu’huyo aliyewahi kutamba na ngoma ‘Kama’.

Mike T
Aliendelea kusema “The kid (Director mpya wa Showbiz) na juzi pia kafungwa.. Alikua anajidai yeye ni Suka wa Clouds FM. 

Wakawa wanakula hela za watu yeye na boss wake (Mike T). Yaani pale ni issue. Kampuni niliyoijenga kwa jasho langu imekufa kius***e

Katika kujaribu kupata ukweli wa upande wa pili wa shilingi tumekutana na jibu rahisi kutoka kwa Mike T “Kuhusu Eryne am not talking anymore coz ishapita now tuangalie kampuni inamove vipi”

Na jana kupitia mtandao wa twitter na Facebook Mike ameandika “Nimeamini leo huwezi kuhitimu kuwa staa bila scandal, nw they pisses me off its time I've to play offense no defense.”

Thursday, May 17, 2012

Solothang na Fid Q kukutana kwenye ngoma moja


Solothang

Pata picha Msafiri Kondo aka Solothang anapokutana kwenye track moja na Fareed Kubanda aka Fid Q ama Ngosha! Ni hit bila shaka.

Basi kwa wapenzi wa hawa jamaa wawili wakae mkao wa kula kwasababu watakutana kwenye ngoma ya Solo.




“Nimepakua ile beat... Sio mchezo aisee!!” ameandika Fid akimwambia Solothang kuashiria kuwa amedownload beat aliyotumiwa na Solo kwajili ya kuingiza vocal.

“That's what I'm talkin about!!! Now will have a #hit na Mimi nature sea haki yake!!!” Aliandika Solo japo hapo mwisho tumeshindwa kuelewa anaamisha nini.

“Shaka ondoa.. Murder nishampanga pia! Ana hamu nayo ile mbaya” aliongeza Fid Q akimaanisha kuwa ameshawasiliana na J-Murder producer wa Tongwe Records ambaye atasimamia zoezi la Fid kuingiza sauti kwakuwa Solo yupo Dublin Ireland.
Fid Q
Mwisho kabisa Solo alimalizia “safi kamanda let's do this for #bongohiphop”

Kama kawaida twitter haina siri, mtangazaji wa East Africa Radio Michael Baruti alidakia “nimefuatilia maongezi yenu weeeeee.... Nyie jamaa mnaleta kitu cha hatari nyieeeee..... Naisubiri tu ofisini.

Unahisi track ya hawa wakali wa Michano itakuaje?

Shilingi 80,000 ndio ulikuwa mshahara wa kwanza wa Lady Jaydee


Ukiwa mtembeleaji mzuri wa twitter kuna mengi kuhusu mastaa utakayoyafahamu. Huko ni sehemu ambayo watu maarufu wanajisikia huru zaidi kuongea masuala yanayowahusu.

Wiki hii Lady Jaydee ameweka wazi mshahara wake aliokuwa anapokea katika kazi yake ya kwanza na ya mwisho katika maisha yake kabla ya kujiingiza kwenye muziki na kuwa mjasiriamali.

“Kazi yangu ya kwanza kuajiriwa mshahara ulikuwa TZS 80,000. Ilidumu kwa miezi kadhaa kazi yangu ya mwisho kabla sijaachana na kuajiriwa," aliandika. 

Hakusema ni kazi gani lakini kwa mujibu wa historia yake ni kuwa aliwahi kuwa mtangazaji wa radio.

Lady Jaydee kama ilivyo kwa wasanii wengine waliokuwa wafanyakazi kama Profesa J, Ray C na wengine, hakuridhika na kipato alichokuwa anapata na hivyo kuamua kufanya muziki ambao leo hii umempa utajiri mkubwa.

Akiwa anamiliki lounge maarufu sana jijini Dar es Salaam ya Nyumbani ameendelea kujiweka vizuri zaidi kifedha ukiachilia mbali fedha anazopata kutokana na muziki.

Kwa wengine mafanikio yake yanawapa wasiwasi ambao kwetu sisi tunaona hauna maana. Katika kutafuta habari zake kwenye mtandao, tumekutana na swali lililokuwa limeulizwa na mtu asiyejulikana katika mtandao wa wiki.answers.comlinalouliza “Is Judith wambura member of freemason?

Jibu lililotolewa kwenye mtandao huo ni “Freemasons do not, generally, advertise the fact they are Freemasons. No public statement can be found by Judith Wambura admitting membership. Therefore any statements made as to membership are speculation.”



Si yeye tu anayehisiwa hivyo kwani tayari Diamond na marehemu Stephen Kanumba wamewahi kuhusishwa na habari hiyo.

Tuesday, May 15, 2012

Facebook yamkera Mo Racka aamua kupumzika kwa muda


Ni mara ngapi umeshawahi kuweka status Facebook na akaja 'mwehu' mmoja kusikojulikana na kucomment ujinga ambao ukaiharibu siku yako na mpaka ukatamani usirudi tena? 

Ni mara nyingi bila shaka. Ili kuwa mtumiaji mzuri wa mtandao huo wa kijamii huna budi kuwa mvumilivu kidogo.

Rapper Mo Racka ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki ameamua kupumzika kidogo na Facebook at least kwa kutoandika chochote baada ya kukerwa na jambo. Hata hivyo uamuzi huo haukuwa rahisi kutokana na jinsi mtandao huo wa kijamii ulivyo addictive.

"Usipokuwa na roho ngumu wallah humu facebook hutaondoka kamwe.

Yaani leo (May 7) nilikuwa nataka kujitoa humu facebook kuna mambo yalikuwa yamenikwaza, mh!! sasa katika kufuata process ndefu za kujitoa mwisho zikaanza kuja picha za rafiki zangu hapa facebook halafu wasichana warembo warembo, juu zimeandikwa majina yao mfano chausiku WILL MISS YOU, Alishaba will CRY, Tricia WILL REMAIN LONELY WITHOUT YOU, Tumtufye won't be happy without you.......
He!! kuona wale warembo na sura zao mbona nimeahirisha... .....ama kweli hapa kuna vi element vya u freemanson..hai wezekani” aliandika Mo.

May 8 mwaka huu akaandika “HII NI STATUS YANGU YA MWISHO YENYE UJUMBE MAALUMU KWAKO..

Maisha Ni PolePole, Ukipata Shida Leo Usilie...Wengi Wapo Kama Wewe Na Hawatoi Chozi...Usikae Chini Na Kulalamika Maisha Magumu...Usiwape Watu Nafasi Ya Kukucheka Na Kuwa Mfano Mbaya Kwa Wengine...Tazama Mifano Ya Waliofanikiwa Na Ufuate Njia Zao Utafanikiwa...Na Umuombe Mungu Akupe Uwezo...Unaweza , Jiamini!!!...Sitokuwepo kwa muda fb” alimalizia.

Angalau ameondoka Facebook kwa kuacha ujumbe mzito unaotupa picha kuwa sasa mtoto huyu wa kishua 'amekua'.

Hata hivyo ukitafuta jina lake Facebook utakuna na akaunti mbili za Mo Racka ambazo zote zina marafiki kibao. Hii ya pili hata hivyo kuna picha zake (hizo chini) alizoziweka May 11 kitu ambacho kinatupa maswali kuwa ameisusia moja na kuendelea na akaunti nyingine ya Facebook? 


Monday, May 14, 2012

Hatimaye Ali Kiba ajiunga na twitter






















Bado hujajiunga na twitter? Ama umejiunga juzi na bado hujazoea? Basi hauko peke yako. Watu wengi tu bado hawaujui vizuri mtandao huo wa kijamii wakiwemo hata wale usiowategemea.

Heri yake Ali Kiba aliyeamua kujikomboa na kuungana na wasanii wengine wengi wa Bongo Fleva waliojazana kule. 

Kwa mara ya kwanza Ali Kiba leo ameonekana akitweet kwa kuandika wale anaowafuata mpaka sasa. Mpaka jioni saa kumi za jioni jumatatu hii, single boy huyo alikuwa ameshatweet mara nane, followers 66 na anaowafollow wakiwa 55.

Wakongwe katika mtandao huo addictive wamemkaribisha Ali Kiba huku wengine wakimalizia na kichekoo!

Katika wakati huu tuliopo sasa, licha ya msanii kujitahidi kuwa na akaunti facebook, ni muhimu zaidi kwao kujiunga na twitter kwasababu huko ndiko wasanii wengi hutumia muda mrefu kupiga soga.

Teddy Kalonga ageukia muziki ama swaga tu!


Unamkumbuka  Teddy Kalonga aka TK? Model wa kimataifa aishie Hollywood, California nchini Marekani. 

Kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja. Kuwa mama hakujazirudisha hustle zake katika showbiz!

Katika page yake ya Facebook kuna picha zikimwonesha akiwa studio tayari kuingiza sauti! 

Maswali yamekuwa mengi kutoka kwa rafiki zake akiwemo Lady Jaydee ambaye ameuliza, “Unaimba bi dada?”

Pamoja na kuwa hajajibu lolote tumeweza kufuatilia picha zake za nyuma na kukutana na picha ya mwaka 2010 kwenye blog  yake mwenyewe akiwa studio na kuandika “K: "Just recently after being back from my home country Tanzania, straight up got back to business. Shown on the pictures, me doing a television voice over for an ad in Los Angeles earlier this week". Praise the Lord Jesus Christ!i


























Maelezo hayo yametupa jibu kuwa kuonekana kwake studio kunamaanisha kuwa anaingiza sauti ya tangazo,documentary ama mambo mengine yanayohusiana na TV. 

Pia inatupa jibu kuwa hajaiacha kabisa fani yake ya utangazaji iliyompa jina nchini kwakuwa mmoja kati ya waanzilishi wa Channel 5!


TK na familia


Saturday, May 12, 2012

Bila milioni 8 Diamond hapigi show mkoani!






















Wewe ni promoter wa muziki na unataka kufanya show na Diamond? Then inabidi ujipange kwanza ili uepukane na mshtuko unaoweza kukusababishia pressure buree! kwa jibu atakalokupa. 

Bila milioni 8 mezani kijana hapigi show mkoani kwako. Na hapo unaambiwa hakuna cha advance wala nini! Anakupa akaunti, unautuma mzigo wote na ndipo unapopata uhakika wa Diamond kuja kwenye show yako.

Kwa mapromoter wa kuungaunga mjini na wenye mitaji ya milioni mbili ndo waseme byebye kwa kijana coz the boy is expensive!

Mtangazaji wa Mbeya Fm Jackline Charles Marandu alipata idea ya kuandaa show na staa huyo wa ‘Mawazo’ na kuamua kumtwangia simu.

Jibu alilokutana nalo hakulitegemea “nimeishiwa nguvu huwezi amini yaani” alisema.

“Nimeongea naye mwenyewe kama nusu saa iliyopita (May 12) Nilitaka afanye show Mbeya ndiyo kanijibu hivyo. Sijajua yuko wapi kwa sasa. Nilitaka kumrekodi ila nikachelewa.Ukitaka show naye mkoani mfano Mbeya utamlipa shilingi milioni 8, utamlipia ndege yeye na utawalipia dancers wake 4 kwa basi”.

Jackline Marandu
Kwa mikoa ambayo ndege haziendi ina maana Diamond ndo wamsahau kabisa kwa sasa? Ama ndo inabidi utafute private jet, makubwaaa!



















Diamond na mshikaji wake Ommy Dimpoz kwenye Kili Awards Academy
Kwa upande mwingine kauli ya Diamond inadhihirisha kuwa Bongo Flava sasa hivi ni biashara serious. Show kama Diamonds are forever na ile aliyopiga pale Dar Live mwezi uliopita vimemuongezea umaarufu msanii huyu anayejituma.

Swali ni Je! Jina lake la Diamond linasadifu uthamani alionao sasa?