Wednesday, May 16, 2012
Mayweather aunga tela kwa Obama, ampinga Manny Pacquiao
Tamko la Barack Obama kuhusu kuunga mkono ndoa za jinsia moja limezidi kupata wafuasi wengi maarufu.
Baada ya Will Smith, Jay-Z na wengine sasa ni Floyd Mayweather.
Tofauti na wengine Mayweather ameamua kumuunga mkono Obama kwasababu tu mpinzani wake bondia Manny Pacquiao wa Ufilipino alisema hadharani kuwa hamuungi mkono Obama kwa tamko lake.
Wakati mitandao mingi imekuwa ikizungumza madongo ya Manny kwa Obama, Mayweather aka Money ameandika msimamo wake kupitia twitter kwa kusema "I stand behind President Obama & support gay marriage." (Nasimama nyuma ya Obama na naunga mkono ndoa za jinsia moja)
Aliongeza "Mimi ni raia wa Marekani na naamini watu wanapaswa kuishi maisha yao watakavyo"
Manny na Floyd hawawezi kukubaliana katika jambo lolote.
Kama wewe ni mpenzi wa Masumbwi. uko upande gani? TeamFloyd ama TeamManny?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment