Jennifer Lopez amesema hana uhakika kama atarejea kwa msimu wa tatu kwenye mashindano ya "American Idol," lakini mtayarishaji mkuu katika show hiyo amesema wanamhitaji kwa kiasi kikubwa.
Nigel Lythgoe ameuambia mtandao wa TMZ, "Tunamtaka tena. Namtaka tena."
Amesema hayo kufuatia tamko la Jennifer katika kipindi cha "Ellen," ambapo alisema, "Sijui kama ntarudi tena kwa msimu wa tatu. Namiss kufanya mambo mengine. Ni kitu ambacho kinakufunga kabisa."
Nigel Lythgoe |
Ameendelea kwa kusema, anaposema "hajui" kama atarejea, ni majadiliano tu, ikimaanisha kuwa milango iko wazi. Karibu Hollywood.
No comments:
Post a Comment