Showing posts with label BONGO SHOWBIZ STORIES. Show all posts
Showing posts with label BONGO SHOWBIZ STORIES. Show all posts

Monday, August 20, 2012

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Diamond





Show ya Mkasi ya wiki iliyopita imetufanya tufahamu mambo 10 muhimu tusiyoyajua kutoka kwa Diamond kama ifuatavyo:

1. Yupo kwenye mazungumzo na label moja kubwa duniani ambao walimtafuta baada ya kufanya show ya Big Brother Africa.

2.Ana simu nne na moja ina line mbili, hivyo ana line tano.Simu yake huiweka silent muda wote kwakuwa zinapigwa muda mwingi. Anayo moja maalum ambayo watu wengi hawaijui.

3. Ana nyimbo 133 ambazo ameshazirekodi tayari.

4.Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.

5.Zamani alikuwa anapenda kurap lakini aliona ukirap huwezi kupata mademu. Alipokuwa akiimba watu wengi walikuwa wanamkataza kwakuwa waliona hawezi.

6. Q Chilla ndiye msanii anayempenda zaidi na muda mwingi husikiliza nyimbo zake.

7. Anamaliza mjengo wake uliopo Tegeta Dar es Salaam.

8.Anapenda kuja kuwa kama Usher Raymond.

9.Anapenda jinsi Dully anawasupport wasanii wachanga kwa kuwashauri na kuwapa moyo kuliko wasanii wengine wakongwe ndo maana anasema huwa hachuji.

10.Maproducer anaowazimia Tanzania Manecky, KGT, Manwalter na Marco Chali.

Sunday, August 19, 2012

MNET wamkubali Martin Kadinda, kumfanyia mahojiano



Kituo maarufu cha runinga cha MNET kilichojigawa katika fani mbalimbali, kimevutiwa na kazi za mbunifu aliyekuja kwa kasi mchini Martin Kadinda.

Mbunifu huyo ambaye ni miongoni mwa wabunifu watakaoonesha mavazi kwenye tamasha la mitindo la Dar es Salaam, DFF, ameandika kupitia mtandao wa Facebook, “True love to everyone... What a great news this Morning... MNET Africa for Martin Kadinda on DFF 2012,” na kuambatanisha screenshot ya ujumbe aliotumiwa na mshkaji wake jinsi MNET wanavyomuongelea.


Saturday, August 18, 2012

Makutano Show: Ruge afunguka ya ndani kuhusu Clouds FM, THT na Antivirus



Katika Makutano Show ya Magic FM Jumamosi hii, miongoni mwa watu waliohojiwa ni pamoja na Ruge Mutahaba wa Clouds FM.

Katika interview hiyo iliyodumu kwa zaidi ya nusu saa, Ruge amezungumza mengi kuhusiana na namna Clouds FM ilivyoanza, THT, namna watu wanavyomchukulia sivyo kwenye muziki na issue ya Antivirus.

Sikiliza interview hiyo hapo chini.

Friday, August 17, 2012

Mastaa wa Mikoa: Tanga wamtosa Zitto, Morogoro waingia mkenge


Habari za kuamika kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai kuwa wasanii wa mkoa wa Tanga wamelikataa wazo la mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe la kufanya wimbo wa pamoja kama Tanga All Stars kwa madai kuwa mradi huo anaufanya ili kujinufaisha kisiasa.

Hivi karibuni Mheshimiwa Zitto alikiri kuutaka urais wa Tanzania wakati wa mahojiano na kipindi cha Makutano cha Magic FM na watu wengi wamekichukulia kitendo cha kuwa karibu na wasanii wa Tanzania kama njia ya ya kujiimarisha kisiasa na kuwashawishi vijana walio wengi nchini.

Leotainment imeongea na MwanaFA kwa simu leo (August 17) ambaye amesema wasanii wa Tanga wana program yao wenyewe iliyopo tangu muda mrefu na wamewahi hata kufanya show za ndani na nje.

Amesema hawawezi kujiingiza kwenye mradi huo wa Zitto kwakuwa umekaa kisiasa zaidi.

Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM mwezi uliopita, Zitto alidai kuwa lengo lake ni kila mkoa kuwa na wimbo wa nyota wenye asili ya mikoa mbalimbali na baada ya Kigoma mkoa wa pili aliokuwa anafanya nao mazungumzo ni Tanga ambao tayari wamemtosa.

Wakati Tanga ikishtukia mchezo huo wenye harufu ya siasa, wasanii wa Morogoro chini ya Afande Sele tayari wameingia mkenge na wamefanya wimbo wa Morogoro All Stars.

Morogoro All Stars inaundwa na Afande Sele, Koba, Stamina, Belle9, Samir, Criss Wamaria, Nassa, Oten, Dayna na Zilla!

Chanzo kimoja cha uhakika kimeiambia Leotainment kuwa mradi wa Kigoma All Stars umegharimu mamilioni ya shilingi.

Amedai kuwa kwenye show ya wasanii hao iliyofanyika mwezi uliopita mkoani Kigoma kila msanii alilipwa si chini ya shilingi milioni moja.

Aidha Mheshimiwa Zitto aliwahi kudai kuwa Kigoma All Stars itakuwa kampuni na inajenga kituo cha kuendelea vijana wenye vipaji mbalimbali mkoani Kigoma.

Kufuatia wasanii wa Morogoro kuja na wimbo wao kama wale wa Kigoma, kumekuwepo na hisia tofauti juu ya miradi hiyo ya wasanii kujiunga na kutoa nyimbo za mikoa ambapo wapo wanaosema ni kitu kizuri huku wengi wakidai inaonesha jinsi watu walivyoishiwa na mawazo mapya.

“Uvivu wa fikra na maisha ya kuiga...wangeweza kufanya kitu nyingine nzuri ya kibunifu kuliko ku-kopi na ku-paste...upu********....kila kukicha tunalala na kuamka kushughulika idea ambayo tayari wenzetu washachomoka nayo..lets not waste time on the same thing always while we can think in wide angle and come up with mo amazing things in the Industry...ghosh....!!!,” alisema mchangiaji aitwaye Likati.

‘Nyerere alikatataa makundi ya ukanda na ukabila nini sasa hii? mimi ni mdau wa burudani Tanzania, hii kitu naona haina maana kabisa zaidi inakuja haribu tu,” alisema mwingine aitwaye Jose Watano.”

Thursday, August 16, 2012

Dully sykes: Mimi ni msanii wa kwanza kupanda ndege Tanzania



Dully Sykes hajaacha tabia yake ya kujisifia ndo maana mama yake alimpa jina la Mr. Misifa. Akiongea na Clouds FM msanii huyo mkongwe amesema yeye ni msanii wa kwanza nchini kupanda ndege. Anasema anakumbuka ilikuwa mwaka 2000 alipanda ndege kuelekea Mwanza ambapo alikaa jirani na Joseph Kusaga ambaye alimwambia Dully  asiogope ndege kutokana na kuwa mgeni kwenye chombo hicho.

Dully pia ambaye kwasasa ameongeza aka mbili ‘Superstar na Hunter’ amesema yeye ni superstar wa kwanza Tanzania baada ya Profesa Jay.

Amesema mwaka ambao Profesa aliachia wimbo wa Chemsha Bongo ndio mwaka aliotoa wimbo wake Julietha na kusema yeye ndiye aliyeitambulisha Bongo Flava nchini.

Aliongeza kuwa ameendelea kuwa pale pale na mafanikio yakiongezeka zaidi kutokana na kumheshimu kila mdau wa muziki bila kujali umri wake.

Fina Mango kumhoji Ruge kwenye Makutano Show wiki hii



Wiki hii kwenye kipindi kipya cha radio cha Makutano Show kinachorushwa kila siku za Jumamosi kupitia Magic FM, mmoja wa mabosi wa Clouds FM Ruge Mutahaba atahojiwa na mtangazaji wa show hiyo Fina Mango.

Kwa namna yoyote interview hiyo itavuta wasikilizaji wengi hasa kwakuwa Fina atakuwa akimhoji bosi wake wa zamani  kipindi anafanya kazi Clouds FM.

Licha ya Fina Mango kuachishwa kazi pamoja na Masoud Kipanya, bado ameendelea kuwa karibu na Ruge ambao wanamiliki pamoja kampuni ya One Plus Communication.

Bila shaka itakuwa interview ya kuvutia.

Unafahamu kuwa ‘Nini Dhambi’ ya Father Nelly ndo ngoma ya Bongo Flava inayoheshimika zaidi duniani?



Jina la Father Nelly litaendelea kukumbukwa daima nchini na wapenzi wa Hip Hop ya Tanzania. Kama ulikuwa hujui ni kwamba ngoma yake ya ‘Nini Dhambi’ ndiyo inayoheshimika zaidi na watu wasiojua Kiswahili duniani wakiwemo wamarekani! 

Licha ya raia wengi duniani walioingalia video hiyo kupitia Youtube na kushindwa kuelewa alikuwa anaimba nini, hiyo ndiyo ngoma ya hip hop ya Kiswahili kutoka nchini Tanzania iliyopewa heshima zaidi kuliko zote unazozifahamu! Comments hizi zinaongea yote. Hakuna video ya Tanzania yenye comments nyingi za watu wa mataifa mengine kama hii.

1.‘Great song, great lyrics. this is hip hop. Simple but powerful
Love from Greece!’

2. Respect and r.i.p to this great poet. I’m novv from the us’

3. This beat is bad ass.. great song, just wish i knew what he was saying!

4. I feel ya pain my nigga!

5. I actually like this even though I don't understand the language I'd rather listen to this than the so called RAPPERS we have in the US

6. I didn't know he was murdered. I am crying.

7. This song always leaves me speechless.

8. Wow this is really good! compare the content of this song with some of the other rappers like Lil Wayne and T.I

9. Is there an instrumental version of this on the internet? If yes, where can I find it? It's epic!
Respect from Norway

10. So nice & lovely..It brings back a lot of memories
real rap real talk no bitches no money no cars this is all about this is REAL RAP.BIG RESPECT FROM USA AND ALBANIA

11. I speak full English and nothing else. I have downloaded a lot of their songs. I have mod idea what they r saying. But duz tht matter? This great music. These guys know how to rap.

Tuesday, August 14, 2012

Agnes Masogange amwomba msamaha Sintah, hakuna beef tena!

Agnes

Baada ya kuwepo taarifa kuwa Agnes wa Masogange alimshutumu Sintah kwa kusambaza video yake ya ngono, imebainika kuwa Aggy amemuomba msamaha na sasa ni amani tu!

Taarifa hiyo imethibitishwa na Sintah kwenye website yake ambaye ameandika:

Sipendi uchonganishi jamani?? huyu dada alishaniomba msamaha na mimi na yeye tunaongea vizuri,,kama mtu anawashwa na yake kupitia funny blogs tafuteni la kuandika.

Wale mliokuwa mnaniongelea kwa Agnes  kaniambia yote nawaangalia tu, mimi simjui Agnes ila nikiona mtu kafanya makosa namsahihisha ndo mana alikuja kuniomba msamaha na sina kinyongo naye nimemsamehe sasa maneno mengine mnayatoa wapi? kama mtu ana picha zangu za ngono zitoeni jamani kwanini mnanitishia??haaaaa nimeshatoka huko kitambooo sana lolest,,labda mtengeneze na za kutengeneza tunazijua hivihivi mtasubiri sana tena sana ninajiamini 100%Agnes alinieleza mkanda mzima wa yaliyomtokea na nikaona wasichana wanadhalilishwa sana kutkana na pombe.
Sintah
Jamani yale maisha ya twendeni tukanywe mbona yamepita? so msiendelezee maneno yenu ya ajabu mimi na Agnes tunaongea tena siku ile ile ndo maana nilifuta posts  na nimemsema sana nadhani ameanza kunisikiliza na akinisikiliza atafika mbali maana ni binti mzuri so mnaopenda watu wagombane poyeeeeeee,, mmeshushukaje??tafuteni mwingine kwangu ni fulllll stooooooop.

Agnes nakwambia hapa mbele ya watu huna marafiki ni wanafiki wao ndio wamenitumia video kwa mda wako uje nikuonyeshe waumbuke  na munch status zako zote walituma 

ONYO KWA MADADA

UWE NA HUBBY WAKO US SIJUI UK NA NCHI NYINGINE USIPIGE PICHA ZA UCHI UKAMTUMIA WANAUME SI WATU NA KWANZA SIKU HIZI MAISHA YA KUAMINIANA YAPO WAPI?                  

JCB ndani ya Star TV Cribs!!!



Crew ya kituo cha runinga cha Star TV leo kinamtembelea rapper wa Arusha JCB Makalla na kufanya version ya superstar Cribs kama ilivyo kwenye MTV Cribs! So hii tuipe jina la Star TV Cribs sio!

‘Leo hii STAR TV wananitembelea hapa home kwangu kufanya kipindi kama mtv crib..nita watag mapicha hamna noma..,” ameandika mtengwa huyo kupitia Facebook.

Tunaamini hilo litakuwa bonge la show!

Monday, August 13, 2012

Diva kutoa msaada kwenye kituo cha New Life Orphan Home siku ya Eid Pili



Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva chini ya mpango wake wa Diva Giving For Charity, anatarajia kukitembelea kituo cha watoto yatima cha New  Life Orphan Home cha Kigogo jijini Dar es Salaam siku ya Eid Pili.

Msikilize zaidi hapa akielezea mpango huo.

Fid Q kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula viazi vitamu

Fid Q enzi za utoto
Siku zote Fareed Kubanda aka Fid ni mtu anayependa kuwa unique katika mambo yake. Leo ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa hapendi kusherehekea kama watu wengine walivyozoea kwa kuangusha party za gharama, kukata keki na kupop bottle kwa sana!

Kuonesha kwamba yeye ni ngoma halisi, Fid atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula viazi vitamu maarufu sana usukumani. Ukichanganya na maziwa ya mgando ama karanga zilizokaangwa, keki  haifui dafu! 

Fid ambaye siku yake ya kuzaliwa leo imemkuta kisiwani Ukerewe, ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM kuwa amejisikia vibaya kukosa kituo cha yatima kujumuika na watoto katika siku yake hii muhimu.

Sunday, August 12, 2012

Exclusive: Diva wa Clouds FM kugombea ubunge wa Kigoma 2015



“Nataka 2015 nikagombanie Ubunge Kigoma , swali kugombania ubunge Kigoma ni Lazima niwe mzawa wa Kigoma? ilov Kigoma,” ni tweet ya mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva aliyoandika saa sita mchana Jumapili hii.

Kama watu wengi walivyomzoea, walijua ameamua kujifurahisha tu kwa kuandika kitu ambacho kamwe hakiwezi.

Lakini Diva alionesha kuwa huo sio utani na kweli amedhamiria. ‘This is not a Joke , nataka kugombania ubunge Kigoma 2015 , Diva future North Kigoma MP, anyone got a Qn, ask! Nantashinda,” alisisitiza.

“Na ntatumia njia inaitwa strength of a woman, u should put that woman first mind games tu and coz got mad lov for kigoma#mpalltheway.”

Kwanini anataka kugombea Kigoma na sio sehemu nyingine? “People wako nice, charming , wanaheshima, wanakubali cha kwao na wana support,” alifafanua.

“Coz Kigoma kuna ardhi, mbuga za wanyama, lake Tanganyika uvuvi and what more??? Vitu vingi sana ,ntasema.”

Amedai kuwa hivi sasa anajifunza Kiha na hivi karibuni ataenda mkoani humo.

“Diva Kigoma future MP, my campaign manager atakuwa@linex_tz , he is training me hicho kilugha cha Kigoma, soon ntaenda.”

Katika kile kinachoonesha watu wengi kumpuuzia kwa kauli hiyo, walimuuliza maswali ambayo mengi yalikuwa ya kejeli lakini alijibu kusisitiza nia yake na kuanza kujinadi.

‘Najua ntaimarisha vipi elimu, ajira na kilimo, nataka wajiajiri na biashara ndogondogo ,mikopo midogo midogo itawasaidia sana.”

“Kwanini nishindwe? Labda nikuulize! Nani kakwambia navaa high heels 247? Nani kakwambia siwezi zunguka vijijini?” alimtupia swali mmoja aliyeonesha mashaka naye kwa kumchukulia kama sista duu!

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wa jimbo ambalo Diva ataliwania kwa madai kuwa yeye atakuwa ‘rais mtarajiwa’ ameonesha kumuunga mkono mtangazaji huyo kwa kusema, “Kila raia mwenye sifa za kikatiba anaweza kuwa mbunge. Bunge linareflect jamii. Acha watu wawe huru kusema watakacho. Hakuna ujinga ulio ujinga mtupu, hata ktk ujinga kuna kujifunza.”

Naye Diva aliongezea, “Am free to say whatever I believe kinafaa. As long As sijamtukana mtu, nasema nautaka ubunge Kigoma by hooks and cooks. Ndo nshachagua huko sasa , no one can fight me or change me, maamuzi, nakutaka sana huko kigoma ndo uamuzi wangu. Mimi sio mzawa ni mzalendo, tunavunja imani ya uzawa ili tulete mabadiliko, ntajiunga na chama kitanipitisha,wananchi watakubali.”

Mjadala uliendelea kuwa mzito. ‘Bado nina mashaka sana kukumbusha tu wanawake wangapi waligombania majimbo wakashinda mpaka sasa ndo tuendelee,” aliambiwa na mtu mmoja nay eye kujibu, “Walishindwa wao, ungenijua ungejua nilivyokuwa na misimamo mikali na sitetereki, nina jiamini, nguzo ya mwanamke kujiamini.”

“Last but not least ! No one can fight me, by hooks and cooks, Diva for kigoma as future MP, vote vote vote , muda ukifika!”

Alimalizia kwa kusema, “It was only a teaser, sneak peak #staytunned2015. #nishatangazania#overthisconvo.”


Thursday, August 9, 2012

Aunt Ezekiel sasa ni Rahma, kuolewa mwezi November



Muigizaji maarufu wa filamu nchini Aunt Ezekiel anatarajia kufunga ndoa mwezi wa 11 mwaka huu.

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa balozi wa Zuku Swahili Movies  tayari ameshavalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake aitwaye Sunday.

Kutokana na hatua hiyo sasa muigizaji huyo amebadilisha dini na kuwa muislam na atakuwa akijulikana kama Rahma.


Sikiliza mahojiano mafupi aliyofanya na kipindi cha Take One cha Clouds TV hivi karibuni hapo chini.

Ney wa Mitego adai mshikaji wake ameshalala na mastaa 3 wa Bongo Movies kwa kuwalipa



Wiki hii Ney wa Mitego amekuwa gumzo la nchi kwenye upande wa Bongo Movies. Katika kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema kila jumanne, Ney amefichua masuala mazito ya jinsi baadhi ya waigizaji wa kike wa filamu nchini wanavyojiuza. Suala hilo ndilo lililopelekea awachane kwenye ‘Nasema Nao’.

Msanii huyo asiyeogopa kuwachana watu maarufu pale anapoona wanazingua, alisema alikuwa na mshikaji wake wa karibu ambaye alikuwa anampenda msichana mmoja wa Bongo Movie. Kutokana na mapenzi yake kwa msichana huyo  jamaa huyo alikuwa akinunua kila movie yake hata kama ikiwa mbaya.

Kuna siku walitoka kwenda klabu moja na mshikaji huyo na kama bahati wakakutana na mrembo huyo. Mshakaji wake aliupiga moyo konde na kwenda kuongea naye bila kujali kama atatoswa ama vipi. Ney anasema haikuwa rahisi lakini baadaye yule msichana alimwelewa na akamwambia hisia zake.

“Kitu cha kwanza kabisa alimuuliza una hela wewe? Yaani ikimaanisha kwamba yeye hana mapenzi yeye ni hela, alimuuliza unaniuzia, akasema no wee huwezi kunipenda mimi. Kwahiyo kama unanitaka sababu umeniona kwenye TV nimekuvutia, tuongee tu nipe hela yangu ntakutumizia ndoto yako.”

Ney anasema mshikaji yule alimfuata kumuomba ushauri na kusema kuwa hela aliyoitaka msichana huyo alikuwa nayo nay eye kumwabia afuate hisia zake. Jamaa huyo alimkabidhi muigizaji huyo hela aliyoitaka na kuondoka naye ambapo alipanda kwenye gari ya Ney akawapeleka  hotelini na kuwaacha.
Baada ya tukio hilo, Ney na mshikaji wake waliamua kufanya utafiti ili kujua kama ni tabIa ya wasichana wengi wa Bongo movies na baada ya wiki moja walimtafuta mwingine. “Naye picha lilikuwa lilelile, kila mtu ana kiwango chake”, alisema Ney.

“Ngoja niwaambie, wewe uliepo kitaani yaani, hebu changa pesa zako nini ukifikia kwenye laki tano au nne…. sababu msichana wa kwanza nakumbuka jamaa alimpa kama laki tano hivi akalala naye mpaka asubuhi, wa pili ambaye mimi nampendaga kwenye movie yaani nikimwangalia hivi huwa najisikia raha, lakini kwa kilichotokea nikabaki kwamba nampenda kwenye movie tu, nikivuta matukio yake tofauti na movie namchukia, sababu wanajirahisisha kihivyo, alipewa laki tatu tu. Kuna msichana wa tatu alidai dola elfu moja lakini mwisho wa siku naye alipewa laki sita.”

Ney anasema ndipo alipoamua kuzungumza kitu hicho na awali alipanga kufanya wimbo mzima kuhusu ukahaba unaofanywa na wasichana wa Bongo Movies lakini aliamua tu kukipachika kwenye ‘Nasema Nao.
Amesema wasichana  zaidi ya asilimia 80 wa Bongo Movies wako hivyo ambapo huingia kwenye fani hiyo ili kupata soko kutoka kwa wadau wa mjini ambao huwatumia kimwili.

Amewataka wasichana wa movie wabadilike ili kusafisha jina la tasnia ya filamu nchini. “Wasafishe ule uchafu uliopo, ili wananchi wakae waseme tunaangalia movie.”

Msikilize zaidi hapa:

Wednesday, August 8, 2012

Sintah amdiss Ney wa Mitego, amuita mshamba asiye na akaunti Facebook



Inaokana Sintah ameamua kuinunua kesi ya wasichana wa Bongo Movies na Ney Wa Mitego aliyewadiss kuwa ni Malaya.

Haya ndo aliyoyaandika kwenye website yake.

“Hivi wa wapi weweee,mbona husomeki weweee,tume google hupatikani wewe. Shukurani kwa mdogo wako alietuletea picha yako ya beach, sijui nani sijui nay utaweza??
Ney wa Mitego
Jipange,namuonea huruma mama yako kuzaa kiumbe kilichoharibikiwa, nina jaribu kugoogle naona Ne-yo wa US sasa nisaidie nitupie kwa mnyamani au kiembe mbuzi niambieeee ili nikupatemy brodaaaaa you have just tickled a private part of a tiger,,, you wanted promonow you gotta maza vitumbua.

NEY WA KUJITEGA MWENYEWE MAANA UNA CHASTE  MBU SIJUI UTAMTEGA NANI, KAMA UNA SHIDA NA MIMI DJ DJ DJ AND MY BRODAA CHOKA ANAJUA NINAPOEGESHA MILONJO YANGU  SASA KAMA UNATAKA KUIKATA KAMA ULIVYOWAMBIA WATU WAKO BBM(MAANA HU HUNA HADHI YA KUKAA KTK MY BBM LIST) MWAMBIE AKULETE.MDOMO HUPONZA KICHWA NA UMEJIPONZA.

LOVES LEO NIMEWAFUNGULIA COMMENT MTU AKIGUSWA ATAJIJUA MAANA NIMECHOKA KUONEA WATU HURUMA KAMA NOMA NA IWE NOMA.NEY NIMESHAMPA RUHUSA MLINZI AKURUHUSU UINGIE SWALI ANAKUJUA??? JIPANGE ULIPOCHOKOZA SIPO KABISA. UNSTOPPABLE.NOTHING BUT CONFIDENCE.

MSICHANA AMBAYE ANA TWO SIDES (COOPERATE FIGURE NA ACTRESS)
OOH SORRY USIJE MCHANA NITAKUWA SERENA NINA APPOINTMENT NA WORLD BANK CREW CONCERNING MY LAUNCH.SINA SHIDA NA  MTU ILA UKINIANZA HUWA NAMALIZA  SHIDA ZAKO.”

Tutegemee wimbo wa New wa Mitego maalum kwa kumdiss Sintah hivi karibuni.

Makala: Wasanii wakongwe onesheni ukongwe wenu na sio kulaumu mnabaniwa

Profesa Jay

Na Emmanuel Msigwa aka DJ Msigwa, Radio Journalist, Radio DJ, Presenter & Club DJ


Neno mkongwe lina maana kubwa sana na kila mwenye kuitwa jina hilo anabeba uzito Fulani, iwe katika nyanja ya kisiasa,uchumi & sanaa na hata michezo. Mtu huyo hutegemewa kufanya kitu kizuri katika eneo lake husika ili liwe mfano kwa vijana wanaotamani kuwa kama yeye. Mathalani mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Italia aitwaye Andrew Pirlo, tumeona jinsi alivyotumia kipaji chake na hasa kuonyesha ukongwe wake katika timu wakati wa michuano Euro iliyomalizika hivi karibuni katika nchi za Poland & Ukrane ambazo ndizo zilikuwa wenyeji wa michuano hiyo,kiasi kwamba kila mmoja wetu amekuwa akilitaja jina lake. Utasikia mtu wa mpira akisema “ Pirlo bwana yule mzee fundi sana” hapa utaona jina mzee limetumika kama mkongwe!
Lady Jaydee
Njoo katika tasnia ya muziki ambako ndiko nilikokusudia kuyaandika haya utakayoyasoma. Hakika nchi yetu imejaliwa sana katika tasnia ya muziki kuanzia ule wa dansi mpaka wa muziki wa kizazi kipya na tunajivunia kuwa na wakongwe katika kila idara. Lakini je, ukongwe wa watu hawa unaleta tija? Unatoa mwangaza kwa vijana chipukizi? Unaonyesha kweli ukomavu wao? Je wanaweza kweli kuwanyooshea vijana hao chipukizi vidole kuwa eneo fulani wanakosea ilhali wao wenyewe wanakosea? Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu wao wenyewe hawaonyeshi ukongwe wao. Hatuoni ukomavu wao ambao tunatarajia tuuone!

Unapotaja wakongwe ambao wapo katika tasnia ya muziki wetu wa kizazi kipya hautakosa kuwataja watu kama Mr II,Lady JD,Prof Jay nk hawa ni watu ambao wamehangaika na muziki huu kuufikisha hapa ulipofikia hakuna ambaye hajui juhudi zao.Hakuna ambaye havijui vipaji vyao. Sote tunakubali kwamba hawa ni majabari ya muziki wa kizazi kipya. Kwangu mimi hilo sina tatizo nalo japo lipo tatizo ambalo mimi  ninaliona na ndilo lilonisukuma kuandika makala hii. Makosa yanayofanywa na wasanii wetu wakongwe! Licha ya ukongwe wao lakini yapo makosa ambayo yanawarudisha nyuma, makosa hayo huwapa chipukizi nafasi za kutokea!

Juma Nature
Mathalani mkongwe Profesa Jay zamani kama Niggar Jay, kwa siku za karibuni naona jamaa kama anatoka nje ya mstari, kwa nini? Nitakwambia na kama nikikosea niambie! Hakuna ambaye hajui uwezo wa huyu jamaa katika kuandika mashairi makali ya hip hop. Ni mmoja kati ya ma legendary wa muziki wetu wa kizazi kipya lakini jamaa anaangushwa sana na kazi zake za video nitakupa mfano, unamfahamu Ryan Leslie? Kama haumfahamu ngoja nikufahamishe machache kuhusu yeye, jamaa ni mwandishi wa nyimbo,mtayarishaji wa nyimbo “ producer” na pia ni mwimbaji, je umekwisha wahi kuangalia baadhi ya nyimbo zake? Unaufahamu wimbo wake unaitwa BEAUTIFUL LIE? Je umekwisha angalia video yake? Kama bado tafuta na uangalie!

Wapo wasanii wakongwe Marekani mmoja wao ni Dr Dre, jamaa kwa ukongwe wake kila anachokifanya  unaona kabisa ukongwe wake unaleta somo kwa vijana chipukizi wa kimarekani. Mbona wakongwe wetu hatuoni ukongwe wenu? Umewahi kusikiliza  toleo jipya la wimbo wa Profesa Jay unaitwa Kamili Gado kamshirikisha  produza Marco Chali? ( ni toleo lake jipya kwa kuwa hana wimbo mpya tofauti na huo) Je umewahi kuangalia video yake? Je inaendana na ukongwe wa jamaa? Ki ukweli HAPANA! Na hapo ndipo makosa wanayofanya wakongwe wetu yanapoonekana.Kwa nini wasanii chipukizi wasiwapige bao? 
Afande Sele
Kama wewe ni mkongwe ambaye tunakutegemea kwanini uuchezee ukongwe wako? Kitu gani ambacho Jay anaweza kukisifia katika video hiyo? Rangi sawa,wale wasichana sawa, uchanganyaji wa picha nao sawa? Vipi kuhusu story board yake mbona ni wimbo ambao unauona kabisa mwenekano wake?
Kama mnaona ni ngumu kutengeneza “kichupa bora” ni bora msiwe mnatoa video ambazo zitashusha thamani ya ukongwe wenu.

Ninyi ni watu tunaowatagemea vijana wajifunze kufanya kilicho bora kutoka kwenu ama sivyo vijana hao watakuwa wanawapiga bao nanyi mnabaki kulia kuwa media zinawabania wakongwe, si kweli, ni ubora wa kazi zenu ndiyo utakaowaokoa iwe audio au video zenu. Kama hazitakuwa bora hakuna atakayewabeba!
Gangwe Mob
Kwa sasa vipindi  vya redio au runinga hakuna anayetaka viwe  vibaya ni lazima viwe  vizuri kwa maana ya kujipatia wasikilizaji au watazamaji, kazi nzuri haiitaji kujua ni mkongwe au chipukizi kafanya, kazi nzuri ni nzuri tu! Badilikeni wakongwe wetu. Fanyeni kazi zenye kiwango kikubwa kulinda ukongwe wenu utakaowafanya muendelee kupendwa daima. Watanzania wana hulka ya kupenda kilicho bora pasipo kujali aliyefanya hivyo ni mkongwe ama la!
Onyesheni ukongwe wenu, teteeni nafasi zenu ili tujivunie ninyi na tuweze kuwanyooshea vidole vijana chipukizi kwa kutoa mifano yenu na wao naamini watakubaliana na sisi na muziki wetu uzidi kuvuka boda hadi boda mkiamua mnaweza sana na nafasi mnayo……………………..kazi kwenu!

Tuesday, August 7, 2012

TID kwenye Mkasi: You wanna put me down to be on top? Sawa go ahead but leave me alone





Wiki iliyopita kwenye show ya Mkasi ya EATV na Salama Jabir, TID alikuwa mgeni na alizungumza mengi kuhusiana na muziki, biashara na maisha binafsi.

Kuhusu mchango wake kama msanii mkongwe kwa wasanii wachanga

It tells me that we have inspired a lot, motivation ilikuwa kubwa tumetoa, mimi sasa hivi nikiangalia one two artist, four artists nasema man, this people are stepping on my stone.

TID anasema wao walijenga msingi mzuri kwa wasanii wa sasa

Akijibu swali la iwapo anaumia kuona wasanii wa leo hawahangaiki kama wao walivyohustle kutoka. Tid alisema: I don’t know, Mungu ana mipango yote, haujui kwanini sisi tumehustle, maybe we gonna get better and better.

Kuhusu Radar Entertainment na Ngwea

Tumeform hiyo band inaitwa Radar Entertainment it’s not such a band, it’s an entertainment company ambayo pia ina band yake inafanya performance pia wanarectruit new artists, give them contracrs, give them a scenario they can improve their lives kama ni talent kweli. Hatutaki gozigozi tunataka tu talent kwasababu we believe we have better talents. Radar entertainment naweza kusema ni Bad Boys Entertainment, we need tha thing. Na kama tunakusign officially, una privilege ya kupata ABCDEFG, siwezi kuvizungumza sasa  hivi lakini am telling you once you are signed with Radar, improvement yako tukikubali we give you status within a minute!

Kuhusu watoto

Yeah I got two kids (mama tofauti) the most recently one ana mwaka mmoja na miezi minne (anacheka) it’s crazy.

Kuhusu mara yake ya mwisho kulia

The last time was the last four weeks, I don’t know I just cried because I felt I was losing it . I felt like losing it because I can see people come telling people , TID hivi story on the radio mimi huyu hajaniona mimi, ts like they all blaming on me and am tryna see why! Kitu gani kibaya nimefanya Khalid mimi.. What's wrong? If you didn’t ask about senseless things am doing no am only devoted my life to this music you know, nini tatazo, why is this all hates, you wanna put me down to be on top? Sawa go ahead but leave me, let me do my life. 

Kama ungependa kusikiliza audio ya mahojiano hayo sikiliza hapa chini.

Chiku K aolewa?



Walisema haolewi mbona kaolewa? Ni Chiku Omary Keto, 28, ambaye jana alionekana kwenye picha alizoziweka kwenye page ya Facebook zikimwonesha akiwa amevaa shela kama Bibi Harusi.

Picha hizo ziliwafanya marafiki zake wa Facebook washangae iweje ameolewa kimya kimya hivyo kama inavyoonekana hapo chini.

Hata hivyo baada ya kumuuliza kuhusiana na picha hiyo alisema ni picha za video ya wimbo wake mpya.

Monday, August 6, 2012

Martin Kadinda aja na ‘Vibunduki Shorts’



Baada ya kumake headline na mavazi yake ya Suti za single button, sasa designer aliyekuja kwa kasi nchini, Martin Kadinda aka Survivor, amekuja na ‘Vibunduki Shorts’.

Ni pensi zenye rangi mbalimbali zenye kitambaa kwa chini kinachofanana na mfuko wa pensi hizo.

Martin amefanikiwa sana kwenye single button na kuweza kuwavalisha mastaa kibao nchini wakiwemo, Diamond, Hemed na Ommy Dimpoz.

Mbunifu huyo ambaye pia ni meneja wa Wema Sepetu, alisema ameuza zaidi ya pair 1,500 za single button.